Ninapata kiungulia kikali nikila maharage, tatizo gani hili?

Hayo maganda ya nanasi unachanganya namaji kisha unachemsha au? Yakisha chemka ndo unachuja hayo maji kisha umachaganya na asali? Asali kiasi gani?
Yes unachanganya na maji then yakichemka unachuja, glass moja ya maji ya nanasi kwa kijiko kimoja cha asali.

Cha msingi usichoke kuchemsha, mimi niliiona uvivu ila nikajikaza now nimepona nakula chochote pilipili yaan kila kitu na nilienda kupima hakuna cha ulcers wala nini.
 
Reactions: BAK
Kwako ulitumia hiyo tiba kwa mda gani wiki wiki mbili mwezi au
 
Kiungulia kinatoka na acid na vyakula kama maharage,nyanya zina acid,sasa je hauna tatizo la vidonda vya tumbo?Kuna wingine wana udhaifu kwenye msuli unaofunga chakula kisirudi kwenye njia kuekea mdomoni,ukiwa na hii hali hata acid ya kawaida tumboni inaweza kurudi juu na kusababisha kiungulia
 
Hii hali inanitokea Sana nikila maharage au nikinywa chai napata kiungulia kwenye tumbo la juu karibu na kifua, nikimalza kunywa chai huwa nakunywa maji mengi ili kizuia maumivu but Kuna muda mpaka unasikia sauti ya tumbo la juu kunguruma.
Sijawahi kupima ulcers but huwa nahisi Ni ulcers
 
Kwa kutuliza kiungulia haraka haraka tumia tangawizi.. Tafuna mbichi.. Mi huwa natumia kila nikiskia kiungulia na kinakata fasta tu
 
Sina vidonda vya tumbo...shida ipo kiungulia tumbo kujaa gesi (ingawa siyo mara zotee) tumbo kunguruma hasa nikiwa na njaa kali
 
Yes ni dalili ya ulcers aliesema kansa ya koo anakutisha.
Hatishwi ndio ukweli, chakula chenye acid kinaporudi juu(regurgitation) kinapounguza sehem ya oesophagus (lower third) kinasababisha squamous metaplasia ambayo inaenda stage ya pili inayoitwa "barrets oesophagus" baaa ya hapo kitakachofuata ni kansa na si vinginevyo.
 
Sio vitisho mkuu,ni kweli,ila baada ya muda mrefu hasa kama hiyo hali ikiwa inajirudia rudia,cha muhimu ni kuacha kula hivyo vyakula vyenye asidi nyingi,ila harage nalo ukilizoe kuliacha ni kazi...!
 
Jamani mpendwa na Mimi nilikuwa na tatzo kama hilo la kuumwa baada ya kula marage sahivi nimetokewa na vidonda kwenye koo vinauna mpaka naskia maskio yanavuta nimetokewa pia na kiuvimbe shingoni cjui ndo mtoki hospital nilienda wakanipa tu pen v nmemaliza Bdo cjapona naomba nisaidie hapo nifanyaje maana naona una utaalamu
 
Heart burn, inanitesa sana hata mimi. Hata nikinywa pombe kali nateseka sana usiku.
mimi mbona na kunywa pombe kali ila haini tesi sema labda asubuhi kama niki chelewa uweka kitu tumboni
 
na hiii huchukua mda gani hdi kuwa kansa maana mimi kuna kipindi ilikuwa too much ila sio kama jamaa, ilikuwa ndani ya tumbo nsikia maumivu sehemu moja upande wa kulia inakuwa kama kidonda kwa ndani hivi hasa nikinywa maji ya baridi ghafla
 
na hiii huchukua mda gani hdi kuwa kansa maana mimi kuna kipindi ilikuwa too much ila sio kama jamaa, ilikuwa ndani ya tumbo nsikia maumivu sehemu moja upande wa kulia inakuwa kama kidonda kwa ndani hivi hasa nikinywa maji ya baridi ghafla
Kansa inatokea baada ya ugonjwa wa muda mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…