Ninapata kiungulia kikali nikila maharage, tatizo gani hili?

Ninapata kiungulia kikali nikila maharage, tatizo gani hili?

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Ndugu wapendwa, naomba msaada wa hii inaweza kuwa nini. Ninapata KIUNGULIA kikali kooni pindi ninapokula maharage. Kawaida KIUNGULIA kina kuwa kwenye kifua. Nikiacha kula maharage hali hiyo inatoweka. Ni Ugonjwa gani huo.
 
Acid reflux. Acha kula maharage, chai, spiced food, soda, kahawa. Kunywa maziwa, tafuna tangawizi na anti acid
Ale tangawizi at the same time umemwambia asitumie spice foods
 
Ndugu wapendwa, naomba msaada wa hii inaweza kuwa nini. Ninapata KIUNGULIA kikali kooni pindi ninapokula maharage. Kawaida KIUNGULIA kina kuwa kwenye kifua. Nikiacha kula maharage hali hiyo inatoweka. Ni Ugonjwa gani huo.
Heart burn, inanitesa sana hata mimi. Hata nikinywa pombe kali nateseka sana usiku.
 
Ugonjwa wako unaitwa Gastroesophageal reflux disease (GERD). Maharage ni acidic in nature sasa inapotokea reflux of that acidic food from the stomach baada ya kula kupitia cardiac sphincter acid hiyo huunguza surface ya oesophagus kwa kua epithelial surface ya oesophagus haiko adapted to acidic substances kama ilivyo surface ya tumbo, hii ni hatari kwani inaweza kukusababishia hali iitwayo barett's oesophagus ambayo inaweza kukusababishia kansa baadae (squamous cell carcinoma of oesophagus) , pia hali hii inaweza kukusababishia vidonda (oesophageal ulcers). Hali hii hutokea mara nyingi mtu anapolala flat baada ya kula au pia anapokula sana na kusababisha mfuko wa tumbo kujaa mpaka juu kabisa.

SULUHISHO
Epuka vyakula vyenye asili ya asidi au tumia vidonge vya kuneuralize acid kabla ya kulala na unywe maji mengi haraka mara tu unaposikia kiungulia ili kuepuka madhara hayo niliyoyaeleza juu
Pia kula chakula kwa kiasi tuu na epuka kulala mara tu baada ya kula au kama inakulazimu kulala basi tumia mto kuinua kichwa kidogo
 
Ukimaliza kula maharagwe lamba na majivu kijiko kimoja au yachanganye kwenye maji unywe uone kama utackia kiungulia.
 
100% ni dalili ya vidonda vya tumbo, nitafute nikupe dawa, karibu sana
 
Duuu mimi tangu utoto wangu napata tatizo hili nikila maharage, mboga yenye nyanya nyingi nk
Mwenye kujua dawa ya uhakika tuambizane jmn (ila kusema tuje pm siyo poa weka hadharan kila mtu afaidike)
Mnaosema dalili za kansa jmn tunatishana mjue [emoji17] [emoji17] [emoji18] [emoji18] [emoji18] [emoji22]
 
Dalili za Kansas??
Duh
Kiungulia kila maharage yaliyo poa nakuta imoo
 
Ndugu wapendwa, naomba msaada wa hii inaweza kuwa nini. Ninapata KIUNGULIA kikali kooni pindi ninapokula maharage. Kawaida KIUNGULIA kina kuwa kwenye kifua. Nikiacha kula maharage hali hiyo inatoweka. Ni Ugonjwa gani huo.

Hiyo ndio dalili ya kupata vidonda vya tumbo ndg yetu, chukua tahadhari kwa kupata ushauri sahihi wa daktari.
 
Back
Top Bottom