Qualifier
JF-Expert Member
- Dec 14, 2012
- 1,252
- 405
Ndugu wana JF mimi ni mtumishi wa umma nimehamishiwa kikazi katika eneo lenye miinuko mikali sana , nimekuta wananchi wa huku wanalima mpunga wa kwenye miinuko (Hill Rice) . Changamoto kubwa niliyo ikuta ikanigusa na kunifanya niandike uzi huu ni kwamba wanachi wanakabiliwa na tatizo la mmomonyoko wa ardhi jambo linalo sababisha rutuba katika mashamba yao ipungue kutoka mwaka hadi mwaka, hali hii imewafanya wavune kiasi kido sana cha mpunga na kuwafanya waishi maisha duni.
Niliwahi kusikia kuwa wenzetu wa kabila la wamatengo wanao ishi kwenye miinuko ya milima ya umatengo huko Mbinga walibuni mtindo wa kilimo cha Ngoro ambacho kinahifadhi mazingira na kuzuia mmomonyoko wa ardhi. Ninawaomba ndugu zangu wote mnao jua aina hii ya kilimo cha NGORO mnijulishe hatua kwa hatua ili tuweze kuwasaidia hawa ndugu zetu pamoja na watanzania wote wanao endesha kilimo katika miinuko ya milima. Ninaamini kuwa humu ndani ya JF wamo wa taalamu wa kutosha kutoa Elimu hii kwa manufaa ya watanzania wote hasa wale wanaoishi na kuendesha kilimo katika miinuko ya milima. NINAOMBA KUWASILISHA