Inategemeana na kesi, mfano ni kesi ya jinai au ni kesi ya madai?
Kama ni kesi ya madai (civil case) hutakiwi kwenda polisi kwa sababu polisi hawahusiki na kesi za madai wala hawaruhusiwi kumkamata mtu kwa kosa la madai (Ingawa in practice wanafanya hivyo lakini sio sahihi). Badala yake nenda Mahakamani moja kwa moja ukafungue kesi au mpe kwanza mdaiwa demand notice (demand letter) alafu muda uliompa kwenye hiyo notice ukiisha hajatekeleza madai yako nenda Mahakamani ukafungue malalamiko au kesi yako.
Kama ni kosa la jinai mfano wizi n.k. anzia kuripoti kituo cha polisi baadae mtuhumiwa atapewa dhamana kama kosa linadhaminika, baadaye atafikishwa Mahakamani.
Kikubwa ujue aina ya kosa au aina ya madai
Kuna makosa au madai yanatakiwa kwenda Mahakama ya Mwanzo, mengine Mahakama ya Wilaya na mengine Mahakama Kuu.