MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nimesikitishwa sana na kitendo cha mwanariadha Mtanzania Gabriel Geay kutomaliza mbio za Boston Marathon na kuachia katikati mara baada ya kuvuka 21km.
Huu ni ukosefu wa uzalendo na kukata tamaa. Hii sio mara ya kwanza kwa kijana wetu kufanya hiki kitendo cha hovyo. Mbio sio kuanza ni kumaliza. Kijana jifunze walivyofanya wakongwe kina John Steven Akhwari na Filbert Bayi...
Mzee John Steven alihakikisha anamaliza mbio huko Mexico akiwa ameumia mguu ambapo kila mwaka familia ya riadha duniani hukumbuka kitendo chake hicho cha kizalendo.
Hata Mzee Filbert Bayi alipoanza kukimbia Marathon kuna baadhi ya mbio alikuwa haingii hata top 30 lakini alikuwa anahakikisha anamaliza mbio. Geay aelewe kwamba sio kila siku atakuwa mshindi au kuingia top ten. Kuna siku zingine huwa mbaya.