Ninatafuta mbia

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Posts
2,401
Reaction score
707
Mimi ni mtaalam wa fani inayoitwa Communication Arts. Nimehitimu chuo kikuu nchini Marekani. Ni bingwa katika kila kazi ninayoifanya.

Baada ya kufanya kazi hapa Dar miaka kadhaa, nimeona kwamba bora nianzishe chuo cha kuwafundisha vijana kile ninachokijua. Tatizo langu ni mtaji.

Nimefanya mahesabu, kwa kuwa pia ni mchumi, nilisomea fani hii. Mtaji wa kuanzia ni Shs. Milioni 30, lakini kama ni mkopo, unarudi wote ndani ya mwaka mmoja na nusu.

Baada ya miaka 5, chuo kitakuwa na uwezo wa kufungua matawi 5 mengine KWA MPIGO.

Ninatafuta mbia, mtu ambaye ni risk-taker makini. Ingawa hii ni anomaly - hakuna risk-taker makini - mimi ninaamini kwamba wapo.

Nitakuwa tayari kuzungumza na mtu ambaye angependa kuwekeza, kwani chuo kitakuwa CHA KIPEKEE na kitapendwa sana na wanafunzi wake.

Mwenye kutaka kuwekeza anitumie Private Message.
 
Mkuu Aidea yako ni nzuri sana ila Maelezo hayajitoshelezi kabisa, kama vipi ungeleta hapa Mchanganuo kwa kifupi watu wangeweza kukuelewa, Haya maelezo yako ni mafupi sana na usiishie kusema mpaka mtu aku PM wew weka maelezo ya kutosha kabisa, make usiseme watakuibia Aidea,

Kwenye AIDEA huwa kina cho ibiwa ni zile techinical issue, jinsi gani ya kuendesha, lakini mawazo ya Biashara huwa ni yale yale ila kinacho ibiwa ni ufundi wa kuendesha au kuunda hicho kitu,

SO MKUU FUNGUKA ILI WAKUSAIDIE
 
Asanteni wote.

Lengo langu kuu ni kuwapa vijana taaluma za kuwa wapasha-habari/watoa-taarifa (communicators). Kama mnavyoelewa, hivi sasa, ili ujumbe wako umfikie mlengwa, unahitaji kuwekwa kwenye mfumo unaoeleweka. Kwa mfano, kuna masuala ya "branding", ambapo kampuni hupenda ujumbe wake uwe kwenye mfumo usiobadilika.

Kuna artistic na technical skills, kama vile produduction (digital videography, editing, motion effects, special visual effects, sound effects, etc.), graphic arts (the full spectrum), na mengi mengine.

Hizi ni highly skilled professions. Kampuni kama vile Tigo, Vodacom, Airtel, hutumia pesa nyingi sana kutengeneza hizo branded advertising campaigns zao, NJE YA NCHI, kwa kuwa hatuna wataalam wa kutosha wenye uwezo wa kufanya kazi hizo KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA. Sisi tumezoea ulipuaji. Angalieni matangazo (graphic ads) ya TBC1, ITV, Channel TEN, na wengineo. CloudsTV wanajitahidi kwenye upande wao wa Graphic Identity.

Mimi nimejifunza kufanya mambo haya kwa kuwa nina kipaji cha asili. Lakini, cha msingi ni kwamba, nataka kuwapa vijana hizi skills, ili waweze kujiajiri wenyewe, ama kwa kushirikiana au kwa namna yoyote ile. Na atakayependa kuajiriwa, basi atakuwa na uwezo wa kufanya kazi yake vizuri.

Nadhani nimeeleweka.
 
Ungekuwa Dodoma ningeingia ubia na wewe kwa kutoa shamba langu la ekari 6.
 
Mlangaja, kuna ulazima gani wa mimi kuwa Dodoma?
 

naomba mchanganuo, wawekezaji wapo.
 
naomba mchanganuo, wawekezaji wapo.

Niko mbioni kuandaa mchanganuo, ambao nitaupeleka Benki. Hata hivyo, najaribu sana kutafuta wabia kutoka sehemu mbali mbali. Nitumie email yako kwa PM, nitakapomaliza mchanganuo nitakutumia nakala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…