Ninatafuta rafiki wa kike atakayeweza kuja kuwa mke hapo baadaye

Llio 002

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
1,636
Reaction score
2,053
Habari zenu,

Naishi Dar es salaam, natafuta rafiki wa kike ambaye baadae anaweza kuwa mke wangu.

WASIFU WANGU
-Nina umri wa miaka 29.
-Nina shahada ya uongozi wa Mauzo na Masoko kutoka C.B.E
-Sina mtoto.
- Nimejiajiri

WASIFU WAKE
-Umri 31 maximum
-Awe mwaminifu na mkweli.
-Asiwe na majivuno na majigambo.
-Asiwe na mme.
-Awe ana jielewa

PM kwa mazungumzo zaidi.

Karibuni
 
natafuta Rafiki wa kike ambaye baadae anaweza kuwa mke wangu
Kama uko tayari kuoa; kama uko tayari kwa majukumu husika - tafuta mke! Kama hauko tayari, anza mahusiano ya urafiki mpaka utakapokua tayari.
 
Ndio maana ya post yangu mkuu
 
Mungu akufanyie wepesi mkuu
Nashukuru Mkuu na mimi nataka nipate furaha ya kuwa na mwenza wa kuniliwaza maana furaha hiyo nimeikosa kwa muda mrefu
 
Uliikosa kwa muda mrefu..ina maana ulishawahi kuoa ukaacha!?
 
Ulipokuwa na girlfriend uliiona furaha?? sasa kwanini ulimuacha na hukumuoa
Mkuu hakuwa mtu sahihi kutokana ni mtu ambaye alikuwa hana focus na maisha yeye kikubwa alikuwa anafikilia ku hangout tu
 
Nimekuelewa. Lakini unajua kuoa is like gambling, unaweza kudhani uliyempata atakuwa mke mwema, matokeo yake akawa pasua kichwa na hapo umeshafunga ndoa, japo sijui wewe ni dini gani. Lakini kama utakuwa mkristo, ukifunga nae ndoa akawa pasua kichwa, moyo wako utapanuka na haitapita muda, uitaiacha dunia hii na utakwenda kwa Jesus au Lucifer! Kwahiyo sasa na shauri utafute binti mcha Mungu, na mwenye hekima. Unaweza kufanya nao urafiki bila kumtangazia nia, kusudi upate muda wa kumfahamu vizuri kabisa kabla hujajitosa mzima mzima kwenye kikaango cha ndoa. Nina miaka 18 kwenye ndoa ndio maana nakuambia maneno haya.
 
Nashukuru mkuu
 
Ila sometimes huwa najiuliza kama mnaoletaga haya mabandiko mpo serious au mnachangamsha jukwaa tu! Mara nyingi huwa sipati jibu kwakuwa wengi huwa hawaleti mrejesho.

Kiukweli mtu uanishi mitaani, unafanya kazi/biashara, unajumuika kwenye mikusanyiko (kanisani, msikitini, harusi, msiba, club, bar, michezoni, sokoni n.k)

Kote huko kweli unashindwa kupata mke mpaka uje utafute mke JF ambapo haumjui mtu hata mmoja? Seriously sijawahi kujua kama huwa mpo serious kwakweli.
 
Bora useme wewe!
 
Habari zenu,

Naishi Dar es salaam, natafuta rafiki wa kike ambaye baadae anaweza kuwa mke wangu.

WASIFU WANGU
-Nina umri wa miaka 29.
-Nina shahada ya uongozi wa Mauzo na Masoko kutoka C.B.E
-Sina mtoto.
- Nimejiajiri

WASIFU WAKE
-Umri 31 maximum
-Awe mwaminifu na mkweli.
-Asiwe na majivuno na majigambo.
-Asiwe na mme.
-Awe ana jielewa

PM kwa mazungumzo zaidi.

Karibuni
Mm hapa na mm nahitaji mtu aliye tulia na mwaminifu maana mm mwenywe n mwaminifu pia
 
Back
Top Bottom