Ninauza Mbolea ya Popo

Ninauza Mbolea ya Popo

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Posts
7,743
Reaction score
13,657
Hello Wadau

Mimi kama kijana Mjasiliamali nimeweza kutembea kwenye Mapango kadhaa na nimefanikiwa kukusanya mbolea ya Mavi ya Popo wa Porini na kiasi kidogo ya Wale wa nyumbani na kuitumia hii mbolea na nimeona matokeo chanya kwenye uzalishaji wake.

Lengo langu sasa ni kuwaridhisha vijana wenzangu hasa wale wa kilimo cha bustani na waumini kindakindaki wa kilimo cha umwagiliaji madini haya adimu.

Kiukweli, mbolea ya popo ni shughuli pevu kwenye bustani na nimeona matunda yake

Hizi ni baadhi tu ya sifa zake kwani ninaitumia kwenye bustani yangu

Mosi, upatikanaji wake ni mgumu sana ndio maana ni adimu na ghali lakini si kama ile ya dukani

Mbili, inatunza ardhi na kufanya mimea yako kupata kiwango kikubwa cha NPK ukilinganisha na mbolea za dukani

Tatu, mbolea ya popo inatibu ardhi dhidi ya magonjwa, wadudu na fungas kwenye ardhi

Mwisho, inawahisha mazao yako kukomaa

KIMSINGI, kama wewe ni mkulima wa bustani na muumini wa kilimo cha umwagiliaji (ndio iliyobaki kuwatoa vijana umaskinini) mbolea ya popo ni msaada mkubwa sana na hutojuta kuitumia isipokuwa ukifanikiwa tu kupata mazao yake hakika utanitafuta na kunishukuru maana hutohitaji mbolea yoyote ile kwenye ardhi kwani yenyewe tu ni 'self-sastifactory'

Kwa wale wanaohitaji tafadhari tuwasiliane kwa kuni-PM

Nawasilisha

Unaweza kupitia links hizi hapa kupata uelewa zaidi

Link 1:
Link 2:
 
Mkuu pamoja na kutuambia mambo mazuri unatukosea. Hujataja bei,ujazo, ulipo na namna tunaweza kuipata mpaka tukuulize. Maana kicha cha uzi hujakitendea haki kabisa.
 
Weka picha Mkuu ya Mavi ya Popo hata kwenye Kisado tuyaone.
 
unge tupia hata vipicha vya bustani zako uzi wako upendezi wadau wana soma na kuupita kimya kimya
 
Back
Top Bottom