Ninavyomkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere: Mwalimu mtu wa watu 1

Ninavyomkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere: Mwalimu mtu wa watu 1

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NINAVYOMKUMBUKA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

MWALIMU MTU WA WATU 1​

Miaka 20 iliyopita baada ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nilimwandikia taazia ambayo ilichapwa katika gazeti la Mtanzania la tarehe 10 Oktoba 2014.

Kuanzia leo nitaweka hapa In Shaa Allah kila siku vipande kutoka taazia hiyo kama kumbukumbu yangu kwa Mwalimu.

''Watanzania tumegubikwa na msiba mkubwa kwa kuondokewa na Mwalimu.
Kwa hakika watu kama Mwalimu huja mara moja katika kila karne.

Mwalimu si kiongozi wa kawaida.
Waandishi wataandika na washairi watatunga.

Lakini hawataweza kumwandika Mwalimu kwa ukamilifu wake.

Mwalimu alikuwa mwanamapinduzi, msomi wa hali ya juu, mtu wa fikra, alikuwa na kipaji kizuri cha kuzungumza na kuwateka wasikilizaji wake kwa nguvu za hoja zake na umakini wa kupanga maneno.

Halikadhalika Mwalimu alikuwa anaingia katika kila tabaka na akawa si mgeni.

Ukimtia katika kundi la watu wa kawaida tu atazungumza kwa kiwango chao na akiwa katika kundi la wasomi hapo Mwalimu anakua yuko nyumbani.

Hakuna utakapomuweka akawa yeye anapwaya.

Wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950 kulikuwa na neno ''kabwela,'' hili ni neno la Kizaramo, maana yake ''karudi.''

Mwalimu aligeuza neno hili likachukua maana nyingine kabisa na neno ''kabwela,'' likamaanisha kuwa mwananchi Mtanganyika anaekandamizwa na ukoloni.

Nguvu ya neno hili lilikuja kuwa kitisho kwa ukoloni wa Kiingereza.

Muingereza akiskia, ''kabwela,'' amesema kadha wa kadha alijua hii ni sauti ya wananchi wanazungumza.

Neno hilo likawa mnyororo uliowaunganisha wananchi wote chini ya TANU dhidi ya ukoloni.
Hii ndiyo ilikuwa falsafa ya Mwalimu.''

Itaendelea...

1570512397487.png

Mwalimu akihutubia wananchi Viwanja Vya Jangwani katika mmoja wa mikutano ya mwanzo ya TANU miaka ya 1950.

1570513693291.png
 
Back
Top Bottom