Ninavyomkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwalimu mtu wa watu 5

Ninavyomkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwalimu mtu wa watu 5

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NINAVYOMKUMBUKA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
MWALIMU MTU WA WATU 5

Mwalimu siku moja katika kuwakumbuka rafiki zake wa zamani, akizungumza na Dossa Aziz na wageni wengine nyumbani kwake Msasani katika kueleza kile alichokiita, ''the TANU spirit,'' yaani moyo wa upendo wa wana TANU, alisema kuwa siku moja wakati wa kudai uhuru alikuwa anatoka nyumbani kwake Magomeni akija Kariakoo kwa miguu akielekea sokoni kutafuta mahitaji yake, lakini mfukoni alikuwa hana hata senti moja njiani akakutana na Mzee Mshume Kiyate.

Alipomuuliza anakwenda wapi, alimfahamisha kuwa anakwenda sokoni lakini hana fedha za kununua chochote.

Mshume aliingiza mkono katika koti lake akatoa shilingi mia mbili akampa.

(Ukitaka kujua thamani ya fedha wakati huo ikutoshe tu kuwa nyumba ya vyumba sita kujenga Kariakoo ilikuwa inagharimu shilingi mia tano).

Kutokana na hali hii Mshume Kiyate aliona itakuwa ni kumtwisha Mwalimu mzigo ikiwa atakuwa anashughulika na kuwatafutia wanae chakula na wakati huo huo anafanya kazi za TANU.

Mzee Mshume akajitolea kuhudumia nyumba ya Mwalimu kwa chakula.
Alifanya hivyo hadi uhuru ulipopatikana.

Baada ya uhuru Mwalimu alimuomba Mzee Mshume aache kufanya hivyo lakini alikataa na akamtafadhalisha Mwalimu aendelee kula chakula chake na kile chakula ambacho kinatolewa na serikali kwake yeye kama mkuu wa nchi alimuomba Mwalimu awape wageni wake.

Baada ya maasi ya wanajeshi Tanganyika Rifles (TR) tarehe 20 Januari 1964 kuzimwa na Jeshi la Kiingereza, TANU ilifanya mkutano mkubwa sana Jangwani.

Mzee Mshume kwa niaba ya wazee wa TANU alipanda jukwaani na kumvisha Mwalimu kilemba kama ishara ya kuunga mkono uongozi wake.

Kisa kingine cha kueleza, ''moyo wa upendo wa TANU,'' ambao Mwalimu ulikuwa haumtoki katika mazungumzo yake na kukieleza kila alipopata nafasi, ni kile alichomueleza marehemu Prof. Kighoma Ali Malima.

 

Attachments

  • MSHUME KIYATE NA JULIUS NYERERE PHOTO.jpg
    MSHUME KIYATE NA JULIUS NYERERE PHOTO.jpg
    38.2 KB · Views: 2
Maa Shaa Allah sheikh Mohammed Said vitabu vyako vinapatikana wapi?
 
Hicho kısa alichoelezwa Kighoma Malima mbona hujamalizia? Au mpaka tukanunue kitabu?
 
Hicho kısa alichoelezwa Kighoma Malima mbona hujamalizia? Au mpaka tukanunue kitabu?
Ndinani,
Hapana hakuna kitabu nitaweka In Shaa Allah hii ni sehemu ya mwisho ya taazia niliyomwandikia Baba wa Taifa miaka 20 iliyopita.

Nilishikika tu na mambo mengine.
 
Back
Top Bottom