Ninavyomkumbuka Maalim

Kipindi hicho alikuwa anaitumia hiyo cafe kufanya mahojiano na vyombo kbalimbali kama voa, nilikuwa naenda hiyo cafe usiku kwani bei ilikuwa rahisi mbali na bei kuwa rahisi internet yake ilikuwa na speed kutofautisha na cafe nyingine
 
Kipindi hicho alikuwa anaitumia hiyo cafe kufanya mahojiano na vyombo kbalimbali kama voa, nilikuwa naenda hiyo cafe usiku kwani bei ilikuwa rahisi mbali na bei kuwa rahisi internet yake ilikuwa na speed kutofautisha na cafe nyingine
Asante kwa maelezo. Ilikuwa imejitofautisha sana ile cafe.
 
Mzee wangu MS,

Habari wa mawaziri Wakristo kuwa wengi kuzidi waislam haimsaidii mtanzania wa kawaida.Mbona sisi wapagani hatuna waziri lakini hatulalamiki?mzee wangu una masomo mazuri sana ya historia shida unamalizia kwa kuweka udini.Sijapata kuona mwandishi mwingine akiweka udini kama wewe Baba.

haya mambo ya udini ndio yanaturudisha nyuma.Baba achana na hii mambo ya kuwaaminisha vijana katika dini.Au kuwaambia vijana dini fulani inaonewa haisaidii zaidi ya kuvunja udugu wetu.
 

Serekali haiwezi kuyafanyia kazi mana hayo hayakuja kwa bahati mbaya, ni mikakati maalumu ambayo ipo. Waislamu always wawe second class citizens kwenye hii nchi.
 
Fedeline,
Unaweza kuwa huoni tatizo kwa waumini wa dini moja kuhodhi madaraka ya kuongoza nchi.

Hili linawezekana kwako kwa kuwa unanufaika kwa hali iliyoko kuwa wewe na ndugu zako wote mmepata fursa ya elimu ya juu na elimu hiyo ikaboresha maisha yenu.

Sasa mfikirie yule ambae toka uhuru anawaona ndugu na jamaa zake wanaishia shule ya msingi na akitazama wanaoingia vyuo vikuu wengi wao ni wafuasi wa dini moja.

Sasa jiweke wewe katika hali hii utaelewa ninachozungumza.

Umezungumza kuhusu Wapagani.

Wapagani kama wapo miongoni mwetu ukiwafananisha na Waislam ni jamii ndogo kushinda udogo kiasi huwezi kuwaona popote.

Na ulipoleta hoja ya Upagani nikawa nimejiridhisha kuwa huna maarifa ya kutosha na hili somo tunalojadili.

Ushauri wangu kwako ni kuwa jifunze historia ya Waislam na juhudi zao katika kupambana na dhulma ya ukoloni.

Ukifanya hivyo utaelewa kuwa Waislam waliongoza harakati za uhuru kwa kutafuta haki na usawa kwa wananchi wote.

Na utaona kuwa hili tatizo la upogo ni suala ambalo limekuwa likielezwa kwa miaka mingi na serikali haijawapa majibu Waislam.

Sasa kueleza tatizo hili si udini.

Udini ni kuzuia wale ambao si wa dini yako kunufaika na fursa zilizopo.

Udugu hauwezi kupatikana katika hali kama hii ya tabaka lililo juu na lingine limekaliwa kichwani.

Wanaotakiwa kutoa majibu ni serikali si "Wapagani," mfano wa wewe ambao licha ya kuwa hampo hamna historia yeyote Tanganyika.
 
Serekali haiwezi kuyafanyia kazi mana hayo hayakuja kwa bahati mbaya, ni mikakati maalumu ambayo ipo. Waislamu always wawe second class citizens kwenye hii nchi.

..kama ni hivyo, suluhisho la tatizo hili ni nini?
 
..kama ni hivyo, suluhisho la tatizo hili ni nini?
JK,
Tatizo kubwa ninaloliona mimi ni kuwa lau kama serikali inajua na kuona hili tatizo lakini kwa kuwa Waislam wenyewe hawajaweza kulifikisha serikalini serikali inahisi iko salama.

Hapa nitasherehesha kidogo.

Waislam ndiyo dini pekee ambayo haina uhuru wa kuchagua viongozi wanaowataka kuanzia mwaka wa 1968 EAMWS ilipopigwa marufuku kuundwa BAKWATA.

Serikali inatambua BAKWATA peke yake kama wawakilishi wa Waislam.
Waislam hawaitaki na haitambui BAKWATA.

Rais Mwinyi yeye katika mambo makubwa aliyowafanyia Waislam ni kuruhusu wakati wa kipindi chake Waislam kusajili taasisi nyingine nje ya BAKWATA.

Tatizo ni kuwa lau kuna taasisi nyingine lakini hizi hazitambuliwi na serikali kama wasemaji wa Waislam.

Kwa hiyo msimamo wa BAKWATA na serikali katika tatizo hili ni mmoja na sawa kuwa Waislam wa Tanzania wana haki sawa nchini na wana fursa zote hawana malalamiko yoyote.

Yapo mengi lakini naamini kwa hayo niliyoeleza hapo ndipo lilipo tatizo.

Kama Mufti wa BAKWATA siku moja tu angekuwa jasiri na kusema kuiambia serikali kuwa Waislam wana malalamiko kuwa wanabaguliwa...
 

..asante kwa majibu yako.

..kwanza, usichoke kutuelimisha kuhusu suala hili.

..pili, kuna maswali ya kukera tunaweza kukuuliza naomba utuchukulie kama watu tunaohitaji kueleweshwa.

..Swali langu ni hili; zaidi ya Bakwata kuna taasisi gani nyingine ya Waislamu ambayo unadhani inastahili kutambuliwa na serikali?

..Naomba utuelimishe kuhusu taasisi mbadala wa Bakwata, na ikiwezekana utueleze viongozi wa taasisi hizo ni kina nani.

..Pia nimekutana na Waislamu ambao wanaamini kuwa EAMWS haikuwa taasisi nzuri kwa Waislamu, kwamba ilikuwa ikikusanya fedha za Waislamu wa Tanganyika na kuzipeleka Mombasa. Waislamu hao wanaamini kwamba Bakwata iko kwa ajili ya maslahi yao.

..Zaidi, sina uhakika kama EAMWS bado ipo, nadhani Kenya wanataasisi nyingine ya Waislamu. Je, EAMWS bado ipo? Na kama ilikufa unaweza kutueleza ni kwasababu gani?
 

JK
Anza hapo to get the gist of the problem:


Ingia na fanya search: mohamedsaidsalum.blogspot.com
 
JK,
Ningependa sana kukupa kila kitu kuhusu BAKWATA sasa hivi lakini inahitaji muda.
 
Mzee wangu Mohammed,

Embu tupe shuluhisho, tufanyeje sasa ili Waisalam waliopigania Uhuru wafaidike? Embu toa shuluhisho ili uache habari ya kupanda chuki kwa sisi tuliozaliwa miaka ya karibuni.

Kuna kitabu nimepata kukisoma. Kinaitwa Shake Hand With A Devil.Kimeandikwa na Dallaire Romeo.

Huyu Bwana alielezea, kuwa jamii ya Wahutu ambao ni wengi Rwanda waliachwa nyuma sana kiuchumi.Sasa in the process wakawapo waaandishi waliokuwa wakichochea kuwa taabu zoote walizonazo Wahutu zimeletwa na Watusi.Kwa kuwa serikali iliyokuwapo madarakani ni ya Wahutu, waliwafumbia macho waandishi na wapiga chapuo wa Kihutu.

Chuki hii iliendelea kukuzwa na ndio iliyozaa mauaji ya Kimbari.Sasa nachelea kusema Mzee Wangu huoni kuwa kuendelea kupiga chapuo hii ya kidini ni kutuletea chuki miongoni mwetu vijana wa leo.Sisi ni aghalabu kuulizana dini zetu.

Na je ni kweli waislam wanabaguliwa kwa sasa? Je kuna vizingiti gani vinawafanya vijana wa kiislam kwa mfano wasindwe kupata elimu? Je una mifano inayoonesha makazini watu wanakosa ajira kwa sababu ni waislam? Vipi kwenye biashara, je waislam wanakosa nafasi za kuuza au kununua kwa sababu ni waislam?

Je mitaani watu wanabaguana kwaudini wao? kama majibu ni sio basi mzee tuache vijana tuishi na vijana wenzetu wa kiislam. Kama enzi zenu mlikuwa na ubaguzi basi usitufundishe sisi tubaguane!!

Mzee wangu hizi dini tumeletewa na Wazungu na Waarabu. Wewe leo hii ni Muislam sababu waliokuwa wanaineza dini ya uislam walifika kwenu mapema babu/baba yako akawaelewa akawa muislam. Yawezekana Wazungu wangefika wa kwanza basi ungelikuwa mkristo.Nitakuelewa tu ikiwa uliingia uislam ukiwa na akili timamu bila ushawishi wa wazazi.Binafsi namheshimu sana mtu aliyeingia dini kwa uchaguzi wake mwenyewe na sio kufuata wazazi wako dini gani.

Hivi ndio kusema uislam/ukristo wako sio jambo la muhimu sana kwako kama mtanzania.Dini za watu hizi. Wewe kuwa muislam ni kudra za mwenyezi Mungu, mwengine kuwa mkristo ni kudra zake huyo huyo Mungu.Maana ndie aliyetaka iwe hivyo.Asingetaka basi asingemfanya mtu mmoja mkristo kwwa kuwaleta wazungu na mwengine mwislam kwa kuwaleta Waarabu.

hubiri mambo ya mbeleni Mzee ili tuishi kwa upendo baina yetu.Italisaidia hili taifa. Usipende kuhubiri mambo ya enzi zenu kwa vijana tusiojua ubaguzi.

BTW: Sisi Wapagani tuna haki, naona kwenye andiko umeona kama hatuna.
 
Fideline,
Wapagani wako wapi?

Walipigania wapi uhuru wa Tanganyika au vita vya Maji Maji?

Yupo jemadari Mpagani kama Abdulrauf Songea Mbano aliyenyongwa na Wajerumani.

Unajua majemadari 62/67 walinyongwa na kuzikwa kaburi la halaiki.

Unajua hakuna hata Mpagani mmoja katika majemadari wale.

Unajua hawa majemadari walikuwa dini gani?
Unajua walichokuwa wanakipigania?
 
Mzee Mohammed,

Sina historia ya imani za majemedari wale.Lakini naamini hawakuwa wakipigania uhuru kwa ajili ya maslahi ya imani zao.Walipigania Uhuru ili kuweza kuwa na usawa katika nchi baina ya wazungu,wahindi na waafrika.Haya ya Imani naona ukiyasisitiza kwa mintarafu ya mtizamo wako.
 
Fideline,
Kumbe hujui historia ya uhuru wa Tanganyika.
Dini imechukua nafasi kubwa sana.

Waislam mchango wao haupimiki kuanzia vita vya Maji Maji (1905 - 1907), kuasisi African Association (1929), Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (1933), TANU (1955).

Kama unavyotishika wewe na waandishi wa historia ya Tanganyika historia hii iliwatisha wakaifuta.

Jifunze uijue historia hii.

Mimi nimeandika kitabu kuiweka sawa historia ya uhuru wa Tanganyika.

Angalia picha hiyo hapo chini.

Kuna vitabu volume tatu historia ya Julius Nyerere na nakala mbili matoleo ya kitabu cha historia ya Abdul Sykes (1924 - 1968).

Abdul Sykes alifutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Jiulize kwa nini?

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Mzee MS

Naona mada imebadilika kidogo ila sio mbaya naona niongezee nondo kidogo hapa

Je kuna umuhimu (wajibu) wa kuanzisha serikali ya kiislam chini ya sharia laws katika Tanzania hii ili kutimiza ndoto au hatma ya wazee wakiislamu waloupigania uhuru tangia miaka ya vita vya majimaji?

Kama ndio, Je hawa wakiristo wa sasa tutabaki nao na dini zao au watabidi waondoke katika ardhi yao na kwenda kwingineko?

Vipi kutakuwa na usawa kwa watu ambao jamii yao haikiwa na ushahidi (documents) za kugombania uhuru kama ilivyo kwa waislam wa kariakoo? Hii na refer kwa namna ulivyomjibu Fideline kuhusu usawa wa wapagani wasivyochangia chochote kwenye historia ya nchi hii na waislamu waliochangua 99.9% katika uhuru wa nchi hii?
 
Shakur,
Tatizo kubwa ni kuwa wengi mnataka kujadili somo msilolijua.
 
mwanzoni nilikuwa na msimamo kama wako, lakini malalamiko ya Waislamu kubaguliwa ktk uteuzi ni ya muda mrefu sasa, na sielewi kwanini serikali haiyafanyii kazi.

Haya malalamiko juu ya mgawanyo wa madaraka kwa vigezo vya dini, jinsia na makabila yalianza kushuhulikiwa kwa dhati enzi ya Mzee Mwinyi . Mwinyi alipopata nafasi ya URAIS akajaribu kushuhurikia malalamiko ya waislam kwa kuwapendelea wao zaidi ya madhehebu mengine na huo ndio wakati marehemu Kitwana Kondo alikuwa na influence sana katika serikali. Kikwete nae alopingia madarakani kama ilivyo ada akaendeleza yale ya Mzee ruksa kwa kuwapa kipaumbele waislam katika teuzi zake kama njia ya kurekebisha hiyo unbalance iliyokuwa inalalamikiwa. Unapoteua watu kwa kufuata dini zao na sio weledi unatengeneza matatizo mengi na haya yalionekana na tunaendelea kuyaona athari nchi ilizopata; mfano mzuri ni matatizo ya Mfuko wa hifadhi ya Taifa[ NSSF] . Mfuko huu uliongozwa kwa muda mrefu na Ramadhan Dau, na ni wakati wa uongozi wake ambapo fedha nyingi za mfuko zilitumika vibaya kwa kuwakopesha wafanyabiashara kama Manji ambao baadae hawakurudisha mikopo!! Pia chini ya uongozi wa Dau Nssf iliwekeza fedha nying kwenye miradi ya majengo ambayo haikulipa kwasababu mingine haikumalizika na mingine Ilikuwa chefu chefu tu kwasababu ilitekelezwa kifisadi!!

Dau ingawa alikuwa ni msomi lakini hakuwa na finacial intelligence ya kusimamia shirika kubwa kama lile, yeye alisomea zaidi mambo ya marketing na ndio kazi aliyokuwa anafanya kule Harbours baada ya Kutoka Chuo Kikuu. Sasa katika kutekeleza hiyo dhana ya religious rationalization ndio wazee wakina Kiwana Kondo wakatumia influence yao na kumteua kijana wao bila kufikiria zaidi juu ya experience na relevance ya education yake to the job!! Ndio maana Dau alipofika tu pale NSSF kama kinara jukumu lake kama alivyopata kile cheo yeye Ikawa kujaza nafasi nyingi na waislam[ kutekeleza religious rationalization] na Ikawa hivyo mpaka alivyomaliza muhula wake!! NSSF mpaka hifi sasa kwasababu ya makosa yaliyofanywa ya kuangalia dini ya mtu badala ya weledi ni shirika ambalo ni mufilisi na kupelekea wafanyakazi wasipate mafao yao mara wanapostaafu!!

RATIONALIZATION ya aina yeyote ile inapotekelezwa ni lazima weledi na uzoefu wa wahusika kupewa kipaumbele!!!
 

..asante kwa maelezo yako.

..lakini wapo Wakristo wengi tu ambao waliteuliwa ktk nafasi mbalimbali na utendaji wao haukuwa wa kuridhisha na wameliingizia taifa hasara.

..mimi nadhani hatua za kuonyesha kwamba "keki ya taifa" inagawanywa kwa usawa zinatakiwa kuwa endelevu.

..siyo jambo zuri kuwa na sehemu ya jamii ya Watanzania ambao wanajiona hawatendewi haki ktk taifa lao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…