kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,015
Ninasikitishwa sana na mbinu za maneno maneno kutoka club yangu ya Simba wakidhani yana msaada wowote katika ushindi.
Nimeona Kaizer chief wameanza kijihami ikiwa ni pamoja na kulalamikia waamuzi.Niliona watu wakishangilia baada ya kuona waamuzi wa mchezo huo kutoka Burundi,na hasa wachambuzi wa michezo ambao siku zote nawaona kama wachawi namba moja wa soka letu.Kuna haja gani ya kuanza kuanika mbinu kama zipo za ushindi?
Mbona jamaa wao walijifanya wajinga ikiwa ni pamoja na waandishi wao wa habari wakiisifu Simba na kujidai wameiogopa,jambo lililowahadaa wachezaji wetu wakajikuta wanashangazwa mapema kabisa.
Kwa ujumla Simba tumefeli kwani tulishindwa kunyamaza na kuanza kuitisha press conference ambayo naona labda ni kwa ajili ya kupata viingilio tu.Sioni kama kweli kuna nia thabiti ya kumtoa Kaizer Chief. Na bahati mbaya,wachezaji wetu ni kama walikuwa na mgomo fulani.Je huu mgomo umeisha?