Mkuu hiyo business inahitaji ujiandae kwelikweli, kwanza kreti tupu hapo lazima zikule pesa si chini ya milioni 2 au 3. maana kwa sasa kleti tupu ni 12,000 sasa piga bia (TBL na SBL) piga soda (coca na Pepsi) ukichukua mia mia maana yake upo kwenye milioni 5 kasoro huko. ukichukua mfano Bia ziwe 50 ukumbuke kuna TBL na SBL na ndani ya hizo kuna categories yaani safari ndogo na kubwa, castle lite, kili ndogo na kubwa, yaani nyinginyingi. Kwahiyo ukichukua chache unajikuta mteja mmoja akija kuchukua kili ndogo kleti 3 tayari ndio kamaliza utakuwa huna kili ndogo hadi uagize. Ni changamoto sana. Anza na mtaji angalau milioni 7 unaweza kufungua kwa kuanzia.