ninaweza kuoa mwanafunzi wangu? nipeni ushauri

itahwa

Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
97
Reaction score
142
naomba ushauri wenu wana jamvi,mi baada ya kumaliza degree yangu kimsingi sikupata kazi katika fani niliyokuwa nimeisomea,so nikawa nafundisha shule fulani hivi ya private ili kujikimu kimaisha,nilifundisha pale kwa miaka miwili,then baada ya hapo nikapata kazi kulingana na fani yangu kwahiyo nikaondoka katika shule hiyo ila kwasasa niko Makerere university nafanya Masters na huku nimekutana na mwanafunzi niliyemfundisha katika shule ile (nilimfundisha form three na four) kwasasa yuko hapa mwaka wa pili,tumeanza urafiki tangu nimefika hapa makerere infact it is going into a serious relationship,kiumri nimemzidi miaka 7 yeye ana 21 mimi nina 28! sasa swali langu ninaweza kuendelea na uhusiano na nikamuoa,tumeshaliongelea hili na yeye ana shida,sasa jamani kuna shida kwa mwalimu kuoa mwanafunzi wake? nipeni ushauri jamani mapema! asanteni
 
Mwanafunzi wako alipokuwa darasani tu!..haina neno kabisa!!

Kuna ticha mlimani alioa classmate wetu, wapo wote mpaka leo!!..labda kama kuna sababu zingine, ila hiyo ni kati ya namna watu wanakutana!!
Take a chance, if you can!!!
 
Mi nadhan kuwa ni mwanafunzi wako sio ishu kubwa, hasa ikiwa age difference ni miaka 7 tu pia hata yeye ni mtu mzima (I mean above 18). labda tungejua ur sex, coz for man marrying a woman younger with age difference of 7yrs is not an issue, and viceversa inaweza kuwa issue.
 
Sioni shida yeyote hapo..
kiumri mmepishana vizuri tu..

So kila lakheri mkuu..
 
Nina jirani yangu mtu mzima tu alinisimulia mume wake alikuwa mwalimu wake wa shule ya msingi na hatimaye wamoana na wana watoto wako chuo.Kaka yangu alimuoa mwanafunzi wake ila ni baada ya kumaliza shule yake, so issue si wewe kuwa ulishawahi kumfundisha ila ni umri kwa huyo unayemuita mwanafunzi wako na upendo wa dhati na si wa kupotezeana muda wala kumkatiza elimu yake. Mungu awasaidie
 
kama kweli una nia ya KUOA RUKSA,
ila kama unaona hapo ni kivuli tu, siyo ruksa hata kidogo.

Kila la kheri ktk mahusiano yenu.
 
Oa mke huyo bana mambo ya shule yashapita umri unaruhusu kabisa
 




Huyo wako kabisa. Ishu ni pale bado mwalimu na yeye bado mwanafunzi wa institution moja.
 
Au ulianza kumfukuzia tangu akiwa anasoma? Ikigundulika ulianza kumzonga tangu utotoni una kesi ya kujibu. Nikuulize swali lingine la kizushi, wakati kako form three hako ka binti kalikuwaje, kalikuwa kasafi sana au kachafuchafu vile na uliwahi kufikiria kama ungekaoa one day?
 
vizuri au vibaya? kwani ni miaka mingapi mnatakiwa kupishana

Mimi hata miaka 20 sioni ubaya
ilimradi msichana awe na miaka 21+
Na kijana awe mkubwa kiumri kuliko msichana
 
Huo ualimu na uanafunzi uko wapi hapo....
 
Reactions: Mbu
Sema nae...muoane! Ila utambue kua ni mwandani wako hivyo yale ya kumtreat kiuanafunzi uache! Tangaza nia mkuu!
 
Sio mbaya kabisa we endelea na process, uhusiano mbaya ni pale unapokuwa bado unafundisha shule na mwanafunzi yupo anasoma
 
chukua chako mapema, ruksa lakini sio kumchezea.
 
kaka kama vipi fanya mipango ya ndoa , hiyo iko sawa hamna tatizo hapo
 
Mwanafunzi wako alipokuwa darasani tu!..haina neno kabisa!!

Kuna ticha mlimani alioa classmate wetu, wapo wote mpaka leo!!..labda kama kuna sababu zingine, ila hiyo ni kati ya namna watu wanakutana!!
Take a chance, if you can!!!

Ni wepi hao...? Wale wa civil engineering? Mwalimu phd akamuoa mwanafunzi wake wa mwaka wa 3 undergraduate katika fani hiyo hiyo.
 
mama Blanca alikuwa msimamizi wangu wakati nafanya research( kwa maneno mengine mwl wangu).......na leo yuko ndani ya nyumba twaishi kama mme na mke.......maisha haya.......ni ruksa mkuu we endelea na process
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…