Ninawezaje kumweleza mtu mwenye shida ya harufu mbaya ya Kinywa bila kumkwaza?

Ninawezaje kumweleza mtu mwenye shida ya harufu mbaya ya Kinywa bila kumkwaza?

Bigmaaan

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2023
Posts
306
Reaction score
699
Habari wadau.?

Yaweza kuonekana ni ulizo la ajabu, ila kwangu limekua gumu.

Kuna mtu ninafanya naye project moja siku ya pili sasa na huja ikatuchukua hadi week moja.

Kazi hiyo inatulazimu tukae meza moja muda mwingi, tukifanya mashauriano na kuchapa kwenye Laptop.

Sasa huyu mwenzangu ana tatizo la harufu isiyopendeza ya kinywa. Kwa muda wa siku 5 zijazo, ninauona ugumu wa kazi.

Ninawezaje kumueleza bila kumkwaza?
 
Nilikuwa na jamaa yangu tupo field Mkoa, tukikaa jirani kwenye kuelekezana jambo kwenye Laptop akawa anatema harufu balaa. Nikamwambia tuu live kwamba una tatizo la Harufu ya Kinywa na nikamshauri ukipiga Mswaki sugua na Ulimi na uwe unakunywa maji mengi.

Tulipomaliza field siku naondoka akasema asante sana umenirekebisha jambo zuri sana.

Mwambie tu ukweli, atachukia siku ya kwanza, then, in long run atakuja kukushukuru
 
Mnunulie Mouth Wash halafu mwambie asukutue kila Mara unapohitaji
 
Habari wadau.?

Yaweza kuonekana ni ulizo la ajabu, ila kwangu limekua gumu.

Kuna mtu ninafanya naye project moja siku ya pili sasa na huja ikatuchukua hadi week moja.

Kazi hiyo inatulazimu tukae meza moja muda mwingi, tukifanya mashauriano na kuchapa kwenye Laptop.

Sasa huyu mwenzangu ana tatizo la harufu isiyopendeza ya kinywa. Kwa muda wa siku 5 zijazo, ninauona ugumu wa kazi.

Ninawezaje kumueleza bila kumkwaza?
Mkuu nipe mimi nimtibie ili aweze kupona maradhi yake ya kutoa harufu katika kinywa.

Nini kinachosababisha harufu mbaya ya mdomo?​


mm

Usafi wa kinywa ni tatizo ambalo wataalamu wanaamini kuwa karibu asilimia 25 ya idadi ya watu duniani wameathirika na tatizo hili. Kuna sababu nyingi zinazochangia tatizo hili, lakini nyingi zinahusiana na usafi wa kinywa.
Harufu mbaya ya kinywa humfanya mtu kuwa na wasiwasi na msongo wa mawazo akiwa katika jamii, ukiongeza unyanyapaa na wao wenyewe wanakuwa na hofu , lakini ni rahisi kushinda shida hii.
Jarida la Afya la MNT limechapisha ufafanuzi, ambao utawasaidia watu wenye shida hii.
Medical News Today inakadiria kuwa mtu mmoja kati ya wanne wana tatizo la harufu mbaya ya kinywa mara kwa mara.
Harufu mbaya ni sababu ya tatu kwa watu kutafuta matibabu baada ya kupata maumivu ya meno.
Pumzi mbaya ni shida ya kawaida ambayo husababisha watu wengine kuwa na wasiwasi sana na kutokuwa na amani. Ingawa, mara nyingi watu hawajui kuwa vinywa vyao vinanuka, lakini wale walio karibu nao wanaweza kuisikia.
Humfanya mtu aone aibu haswa wakati anajua mdomo wake unatambulika kwa harufu nyingi.
Harufu ya mdomo inaweza kusikika ukiwa mbali ya mita nne mara nyingi.

Ni nini kinachosababisha harufu mbaya ya kinywa?​

Pumzi mbaya inaweza kutokea ikiwa mdomo haujaoshwa vizuri, na wakati mwingine inaweza kuwa sababu ya ugonjwa.
Pia, kuna aina fulani ya vyakula ambavyo vinaweza kusababisha harufu mbaya ya kinywa.
Na maadili kadhaa ya kawaida yanaweza kusababisha pumzi mbaya.
  • Ni shida inayoathiri mtu mmoja kati ya watu wanne
  • Sababu kuu ikiwa ni usafi duni wa kinywa
  • Kuacha mabaki ya chakula husababisha shida hiyo
  • Kuoza kwa meno
  • Kuweka kinywa chako kuwa kikavu
  • Kuvuta bangi kunaweza kusababisha harufu mbaya mdomoni
  • Pia kuna visa ambavyo dawa za matibabu zinaweza kusababisha harufu mbaya lakini ni suala la muda tu kabla ya kumaliza dawa hizo
  • Pia kuna maambukizo ambayo huathiri zoloto na pua na mdomo ambapo bakteria huoza na kusababisha harufu mbaya ya kinywa.
  • Vyakula vya familia kama vitunguu, vitunguu na pipi husaidia kupunguza harufu.
kinywa

Je! Unawezaje kutatua tatizo hili?​

Njia ya kwanza ya kukabiliana na harufu mbaya ni kuweka kinywa chako safi kwa kupiga mswaki mara kwa mara baada ya kula na wakati wa kulala.
Ikiwa hauna brashi, hautaweza kupiga mswaki au kupiga mswaki kila wakati unakula, kwa mujibu wa madaktari.
Nenda kwa daktari wako wa meno mara kwa mara ili kujua ikiwa kuna meno yoyote yameharibika na yanaweza kusababisha harufu mbaya ya kinywa. Kumuona daktari wa meno mara mbili kwa mwaka inatosha.
Ni vyema kuosha kinywa chako na maji ya vuguvugu na chumvi kwani inaua vijidudu mdomoni mwako ambavyo vinaweza kusababisha harufu mbaya ya kinywa.
Chukua tahadhari kwa kuondoa chakula kutoka kinywani mwako.
Linapokuja suala la kupiga mswaki, safisha ulimi pia.
Epuka kuruhusu kinywa kukauke. Kunywa maji mengi hupunguza homa hata ikiwa haujala chochote wakati wa mchana.
Epuka kuvuta sigara au vileo vingine.
Kula bigijii haswa pipi zisizo na sukari
Ikiwa mtu amejaribu hatua hizi zote nyumbani na mdomo hauachi kunuka basi kuna haja ya kuonana na daktari, haishangazi kuna meno ya kuoza ambayo inahitaji kuondolewa.
Mambo 5 ya kufanya kuepuka harufu mbaya na magonjwa ya fizi
m
Baadhi ya watu husema unapaswa kupiga mswaki mara mbili kwa siku.Lakini wataalamu wa tiba wanatoa maelezo zaidi juu ya mambo muhimu unayopaswa kuyafanya kuzuwia harufu mbaya mdomoni, kuoza kwa menona ugonjwa wa ufizi.
Haya ni baadhi ya mambo unayofaa kuyafanya:
Usisukutue mdomo wako mara moja baada ya kupiga mswaki
Mamlaka ya huduma za afya nchini Uingereza (NHS)inashauri baada ya kumaliza kupiga mswaki, unapaswa kutema dawa ya mswaki ya ziada, lakini usisuuze kinywa chakomara moja, kwasababu kwa kufanya hivyo unaondoa Floride iliyomo ndani ya dawa hiyo itapunguza haraka kabla haijafanya kazi yake.
Usitumie vijiti kuondoa chakula vilivyokwama kwenye meno.
m

NHS inawashauri watu wasitumie vijiti kuondoa vyakula vilivyokwama katikati yameno, maana vijiti hivi vinaathiri ufizi na kuweza kusababisha maambukizi
Wanashauri utumie brashi zinazoweza kusafisha katika ya meno kama una mianya katikati ya meno yako.
Tumia uzi kupunguza harufu mbaya kinywani
Wataalamu wanashauri kutumia uzi wa Flossing fit ambao unaweza kuuweka taikati ya meno yako na kuuvuta mbele na nyuma ili kuondoa mabaki ya vyakula yaliyokwama yanayosababisha harufu mbaya kinywani. Hata hivyo wanashauri kuwa utumiaji wa uzi wa mara kwa mara sio mzuri kwa afya ya kinywa.
Tumia dawa ya maji ya kuosha kinywa baada ya kubrashi meno
NHS inashauriwatu watumie dawa ya kuosha kinywa baada ya kupiga mswakibadala ya maji ili kuepusha kuondoa dawa ya floride ambayo husaidia kusafisha kinywa.
Unapaswa kuwasaidia watoto kupiga mswaki hadi watimize umri wa miaka 7
m

NHS inawashauri watu kuwasaidia watotokupiga mswaki hadi watakapotimiza umri wa miaka saba. Kulingana ushauri huo, iwapo hautawasaidia, hautaweza kufuatilia na kuwafunza kusafisha menohawataweza kukumbuka kufanya hivyo mara kwa mara
 
Mwambie tu kwa upole kuwa kinywa chako hakipo sawa.

Akamuone Mtaalamu wa Afya ya Kinywa atamsaida kumchunguza na kumpa tiba stahiki ya harufu mbaya mdomoni
 
From dar es Salaam
Amwambie daah mwanangu mtu ni afya na ukiona kwenye mwili wako kuna utofauti kidogo kiafya usi subiri watu waje kukuambia inge kua vizuri tuka fanye checking ya mwili, na mimi nilikuwa na tatizo km ilo lakwako
 
Amwambie kuna mouthwash nzuri zimetoka , waende wote wanunue pamoja then huyu muhusika atatumia ila aliyemuambia atachagua atumie au lah.
 
Back
Top Bottom