Ningekuwa kiongozi mkubwa, leo hii serikali ya mkoa wa Kilimanjaro na baadhi ya idara wangepata misukosuko isiyosahaulika

Sasa kama hakufuata taratibu. Tufuate taratibu na tutii mamlaka .
Yaani unajua kimtindo unaudhi sana bro au wewe ndio yule ofisa wa TIC aliyejibu jana labda hujui impact ya yule mkulima akiamua kususia na kuondoka nchini!!
 
Kwakweli mkuu yaani pamoja na madhaifu yake yoote aliyokuwa nayo lakini kwenye mauzauza kama haya ungesikia mtu katumbuliwa kesho yake inakera sana yaani!!
 
Ukweli ni kwamba kama tukiwarahisishia hawa wawekezaji mazingira yao ya kutenda kazi zao kwa namna nyepesi, yaani kila idara ikitatua changamoto zao kwa wakati na kwa umakini na KUONDOA kero za kijingajinga tutaondoa tatizo la ukosefu wa ajira hapa nchini kwetu kwa kiwango kikubwa sana.
 
Ule mkoa Haina viongozi ni mapoyoyo tu.
 
Na bahati mbaya nyingine tuliyonayo ni kuwa kilimo kimepuuzwa sana hapa nchini licha ya kuongoza katika kuzalisha ajira, kutupatia chakula, kutuletea fedha za kigeni, zaidi ya hayo kilimo kwa nchi yetu ni field rahisi sana, kwani tuna ardhi nzuri Hali ya hewa nzuri tuna mito maziwa bahari mabwawa, lakini pia tunazungukwa na nchi zenye changamoto lukuki ambazo kilimo chetu kingetoa majibu.

Lakini kwa kupuuza huko hata magazeti ya leo sijaona lililoripoti hiki kisa cha mholanzi ili kuwaamsha watendaji toka usingizini. Mimi ningetazamia watu wangepumzisha porojo za siasa hii kero ikajitokeza kwenye front page ya magazeti yetu yote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…