kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Unapotamani mfanyakazi wa hospitali a-smile kwa mgonjwa kuna mambo mengi sana lazima afanyiwe kabla ya kukutana na wagonjwa. Miongoni mwa mambo hayo ni mahali pa kuishi karibu na hospitali.
Wafanyakazi kazi wa Muhimbili pale wanaishi mbali sana, wanatoka na kurudi usiku sana kutoka na kufika na nyumbani na hospitali respectively. Nguvu na tabasabu zao zote zinaishia barabarani wakati wa kwenda na kurudi kazini.
Kwanini serikali isingefikiria kuwapa nyumba zile au kuwajengea watumishi wa afya nyumba kama zile karibu na hospitali? Tumeona maghorofa kwaajili ya askari, watumishi wa afya je?
Mtumishi wa afya anatoka Chanika kwenda Muhimbili kila siku, utategemea nini anapokutana na mgonjwa? Amechoka, anasinzia na ana njaa.
Vipaumbe vyetu vyote vimekaa kisiasasiasa na kiuchaguzichaguzi, tutachelewa sana.