Mhafidhina07
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 3,340
- 4,659
Salaam wanajenzi.
Natambua kuwa nchi yetu ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa (UN), umoja wa kikanda (SADC na EAC) ambapo kwa pamoja wameridhia kuongoza kwa kutumia katiba za nchi zao ambazo zimedhibiti sheria za kikanda na kibara kama ilivyotanabaishwa katika mfululizo wa vifungu na sheria za kimataifa mfano uhuru wa habari, uhuru na haki za binadamu pamoja na uhuru wa asasi za kiraia na vyama siasa.
Mwanasiasa mkubwa ambaye anadhama ya cheo anaropoka hadharani kwenye kipindi karibu na uchaguzi mkuu na kuzua taharuki kwa raia,ni dhahiri kuwa amevunja na kuivua heshima ya serikali ya CCM pamoja na rais wake.
Si hivyo tu, pia Nape Nnauye ameiabisha na kuidhalilisha tume ya uchaguzi na watendaji wake, amedhalilisha mfumo mzima wa utawala/siasa.
Binafsi naona kuna ulazima wa kung'atuka kwenye nafasi aliyopo anaipaka tope taasisi na cheo cha waziri wa habari.
Nakumbusha.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!