Ningependa kufaham historia ya uhindu, Tafadhali

Ningependa kufaham historia ya uhindu, Tafadhali

bartaizo

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2013
Posts
236
Reaction score
91
Ndugu wapendwa naomba kujuzwa kuhusiana na imani ya uhindu

2 Timotheo:4.2
lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
 
Uhindu ni dini kubwa yenye asili katika Bara Hindi .
Ikiwa na wafuasi milioni 900 ni dini ya tatu baada ya Ukristo na Uislamu kwa wingi wa waumini.
Nchi zenye Wahindu

Katika nchi za India, Nepal na Morisi na kwenye kisiwa cha Bali (Indonesia) wakazi wengi hufuata aina mojawapo ya Uhindu.
Vikundi vikubwa viko pia:


Bangladesh (11 millioni),
Myanmar (7.1 millioni),
Pakistan (3.3 millioni),
Sri Lanka (2.5 millioni),
Marekani (2.0 millioni)
Afrika Kusini (1.2 millioni),
Uingereza (1.2 millioni),
Malaysia (1.1 millioni),
Kanada (0.7 millioni),
Fiji (0.5 millioni),
Trinidad na Tobago (0.5 millioni),
Guyana (0.4 millioni),
Uholanzi (0.4 millioni),
Singapore (0.3 millioni)
Surinam (0.2 millioni).

ASILI.

Neno Hindu linatokana na lugha ya Kisanskrit ambapo Sindhu ni jina la kale la
mto Indus uliopo kwenye sehemu ya magharibi kaskazini ya Bara Hindi. "Hindu" imepatikana mara ya kwanza wakati wa karne ya 6 KK katika andishi la mfalme Darius I kwa maana ya "watu wa ng'ambo ya mto Indus

Hapa "Sindhu / Hindu" haina maana ya kidini bali ya kijiografia pekee.


Katika Kiajemi neno "Hindu" linamaanisha wakazi wa Uhindi pamoja na wafuasi wa dini kubwa ya nchi hiyo. Mnamo karne ya 11 milki iliundwa na Waajemi katika Bara Hindi iliyoitwa "Hindustan" na mji mkuu ulikuwa Lahore.


Baadaye Waingereza walipokea jina hilo kutoka Kiajemi, wakilitumia kwanza kwa nchi na baadaye hasa kwa wafuasi wa dini zisizo za Kiislamu , Kiyahudi wala Kikristo. Jina Hinduism (iliyoandikwa mwanzoni Hindooism ) lilikuwa kawaida tangu karne ya 18 kwa kutaja falsafa na dini zenye asili ya India.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom