Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KUKU "MAKANGE RECIPE" (MAKANGE CHICKEN) IRINGA
Wakati ni wa chakula cha mchana na niko katika mgahawa mmoja katikati ya mji wa Iringa jina lake Coffee Shop.
Mwanangu anatoa "order," anaomba kuku wake atengenezwe "Makange."
Mimi ikawa nimesikia kama kasema "makande."
Nimesikia hivyo kwa kuwa tuko sehemu ya maakuli na makande ni aina ya chakula.
Ndani ya nafsi yangu ikawa nimeguna kimoyomoyo nikijiuliza, "Huyu bwana toka lini kaanza kula makande?"
Mbali ya kujiuliza kama kuna hoteli wana makande kwenye "menu.''
Nilipomuuliza akaniambia yeye ameagiza, "Kuku Makange."
Ndipo haraka ikanijia kuwa kuku wa marehemu Robert Makange amewasili Iringa.
Nikamuuliza huyu mwenyeji wangu kama anamjua Robert Makange.
Hakuwa anamjua.
Nataka kumweleza nani Robert Makange yeye tayari keshawasiliana na Mwalimu Google namsikia ananisomea, "Robert Makange muasisi wa Kuku wa Makange..."
Kidogo sikupenda.
Yaani Robert Makange anatambulishwa na Prof. Google kwa kuku wake watamu na si kwa kuwa alipigania uhuru wa Tanganyika?
Ningependa kufahamu kama kuna hati miliki ya Kuku wa Makange.
Picha ya kwanza ni Robert Makange mmoja wa wahariri wa gazeti la Mwafrika.
Picha ya chini ni ''Makange Chicken.''