Nini anatufunza Rais huyo katika ulimwengu wa leo?

Nini anatufunza Rais huyo katika ulimwengu wa leo?

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
photo_1313861665973-1-0.jpg
2011-08-20T181834Z_01_BTRE77J1EWP00_RTROPTP_2_USA.JPG

U.S. President Barack Obama walks out of the Bunch O Grapes bookstore
after shopping with his daughters in Vineyard Haven on Martha's Vineyard
in Massachusetts August 19, 2011. REUTERS/Kevin Lamarque

Viongozi wengi wa Kiafrika wakishapata madaraka makubwa huwa miungu wadogo kiwango cha kuhusuju utwa na utwana. Kiwango hiki cha Obama kwenye bookshop na watoto wake kununua vitabu tena toka pesa ya mfukoni viongozi wetu wanapaswa kujifunza. Na kwa vizito wetu wa kibongo hapo angefunikwa na utitiri wa viongozi wa ngazi zote kumpokea na kumsindikiza. Viongozi wetu wakishakabidhiwa kuongoza dola basi walipakodi wanawajibika kwa kila kitu hata kumnunulia wembe wa kunyolea ndevu, na kama ni mwanamke basi serikali itawajibika kuandaa saloon kwa gharama yo yote.
 
Hapa tunajaribu kuangalia kiti anachokalia Rais na majukumu yake na awapo nje ya kiti cha urais awapo katika shughuli au mapumziko yake binafsi anatakiwa aweje? Sijabahatika kusikia kiongozi wetu wa nchi anachukua likizo kwenda mapumziko, nilizoea kuona haya kipindi cha Mkapa. Inaashiria Rais wa sasa mapumziko yake huunganisha na safari zake za Ki-Vasco da Gama? Lini ataenda kupumzika Bwaga-moyo na kujikumbusha kuogelea na kutembelea maeneo ya Kaole, soko la watumwa na kule Kizuiani kuona nyumba za makumbusho walikotunzwa watumwa walionunuliwa toka kwa waarabu na kuwalinda wasichukuliwe tena?

Siku Rais wa Tanzania akiingia dukani na kuchomoa pesa yake mfukoni kununulia mahitaji ya familia itakuwa historia, maana pamoja na mishahara yote hii na malupulupu bado kuna bajeti ya matumizi mengine binafsi ambayo wabunge wanalazimishwa kuidhinisha na posho yake haiguswi. Huu mtindo si kuwanyonga zaidi walipa kodi wenye hali ngumu ya maisha?
 
viongozi wetu wanachanganyika na wananchi kwa kualikwa
wawe wageni rasmi wa mashindano ya urembo na wapate kuchagua....

wanunue vitabu,wana muda huo??????
 
viongozi wetu wanachanganyika na wananchi kwa kualikwa
wawe wageni rasmi wa mashindano ya urembo na wapate kuchagua....

wanunue vitabu,wana muda huo??????

Kinachonikuna hapa Rais mwenyewe kuichukua familia yake na kwenda shopping na kutoa hela yake ya mfukoni, wakati viongozi wetu kila wanachotumia ni cha mlipa kodi, mshahara na malupulupu yake hayagusi, sasa hizo pesa analipwa kwa ajili ya nini kama hatumii kwa matumizi kama hayo?
 
Utitiri wa viongozi kuandamana na mkuu ni gharama kiasi gani tunatumia? Angalia obama alipo ni vigumu kujua nani ni shopper na nani ni kachero. yuko huru na familia yake kama wewe na mimi tuendapo shopping.
 
Jamani katika nchi zetu hizi mnazungumzia raisi tena, hapana, funga kazi ni mke wa raisi anayetembea na misafara ya magari 20!!
 
Mbona anatembea huru bila utitiri wa viongozi kama mwuza sura. Vasco da Gama hapo angeandamana na makamu wa rais, waziri mkuu, mawaziri kadhaa, manaibu kadhaa , mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na wakurugenzi kibao licha ya utitiri wa intelijensia na bila kuwasahau wale polisi washika magobole.:msela:
 
Atawatembelea vip watu ambao hawajamchagua. Kura wamechakachua.
 
Nimeshakutana na JMK Mlimani City ndani ya games anapiga shopping taratibu, bila waandishi wa habari bila vurugu. Kama kawaida yake hana makeke, action speaks louder than words!

Kikwete tumeshasikia pia akiwa likizo binafsi, nani ambae hajasikia? mnanchekesha.
 
Back
Top Bottom