Nini asili ya jina Tanganyika na Nani alilitunga jina hili?

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
Kumekuwepo maswali ya watu wengi wakitaka kujua ASILI ya JINA la TANGANYIKA.

Ili kuweza kuhakikisha mjadala unakuwa endelevu na msomaji anapata majibu sahihi, tumeonelea ni vema kuweka mjadala huu kwa pamoja:

ILIANZA HIVI:
Jamani nimekuwa nikijiuliza sana jina la Tanganyika lilitokeatokea vipi, kama lilitungwa ni nani aliyelitunga na maana yake ni nini. Naomba wataalamu wa historia wanijuze tafadhali.

=============
Baadhi ya maoni:


 
mwalimu wangu wa historia aliniambia.
Limetokana na mzungu m1 aliyekua anajaribu kuelezea wasomaji wa kitabu chake alichokiandika.
Alikuwa anawaelekeza sehemu ambapo raw materials znapatikana.
Akawa anasema.

From tanga to nyika land .
Mean interior of Tz.

Ndo ikawa inaitwa
Tanganyika.
 
Nikirejea historia, kabla ya kuja kwa wakoloni, hapakuwa na tanganyika kama nchi. kulikuwa na jamii za wabantu aambazo zilikuwa na tawala zao kamili. Baadhi ya tawala hizo ni:
1. Milambo Kingdom
2. Yao kingdom,
3. Buha kingdom.
4. Bahaya kingdom na nyingine nyingi. hapakuwa na jina jina tanganyika kama nchi.

Wapelelezi(explores walipofika katika maeneo haya, walianza kusign mikataba ya kutwaa maeneo ya east Africa. eneo lote kutoka kigoma, likapewa jina tanganyika jina lililokuwa likitumiwa na wenyeji wa kigoma/ujiji- kuita eneo lao lilikuwa na maji ya kutosha ndilo ziwa tanganyika.

hivyo hata wakati wa kudai uhuru, kwa kuwa maeneo yote yaliyokuwa chini ya mjerumani yalitambulika kama tanganyika, hata wapigania uhuru walibaki kulitumia jina hilo kwani tayari lilikuwa limeshazoeleka sehemu tofauti za ardhi yetu.

nawasilisha tafadhali.
 
Mwanakili90

Huyu mzungu alikuja lini, kwa hiyo ina maana kabla huyu mzungu hajaja hatukuwa na jina? Kama tulikuwa nalo lilikuwa lipi kuna anayeweza kujua.
 
Last edited by a moderator:
Kuna sehemu kati ya Muheza na Tanga katika Mkoa wa Tanga ambayo inaitwa Tanganyika inawezekana ikawa ndiyo chanzo cha jina hilo kutumika kwa nchi nzima.
 
Huyu mzungu alikuja lini, kwa hiyo ina maana kabla huyu mzungu hajaja hatukuwa na jina? Kama tulikuwa nalo lilikuwa lipi kuna anayeweza kujua.
Kaka nadhan umepata pcha jnsi lilivopatikana.

Kabla ya kujulikana ilo kuliku kunaitwa interior from indian ocean.
Then huyu mzungu ndo akaja na jinsi yake ya kuelezea.
Mean from Tanga to nyika land.
Maana alikutana na majan maref na mapori ambavyo coast hayakuwepo ambayo na wenyej waliziita nyika thats y akawa anatoa direction kwamba ukiwa tanga then u move to nyika land.
Ndo Tanganyika ikawa created ivyo.
 
Asante ntagunga kwa mchango wako, kwa hiyo maana hasa ya neno tanganyika ni maji au nini? Na kwa nini kigoma ikawa maarufu zaidi kiasi cha jina kutoka huko kuwa maarufu zaidi mpaka kuruthisha nchi nzima kuitwa hivyo?
 
Last edited by a moderator:
mhh,which z which!? Inasemekana jina tanganyika lilitoka na neno Sanganigwa(karibu,according to waha),wakati huo alifika Mzungu fulani maeneo ya ujiji na wakazi wa huko wakawa wakimlaki hivyo,sanganigwa..inasemekana alishindwa kutamka kwa ufasaha,akaishia kusema tanganyika(sanganigwa),.ofcourse mimi hii naiona somehow true kuliko nyingine za kuunga unga..
 
Ukifuatilia sana utagundua nchi yetu ilikuwa vipande vipande
Mfano nzuri ni Kilwa, ilikuwa ni nchi kamili ambayo ndiyo
ya kwanza kwa A.Mashariki kuanza kutumia fedha zake
yenyewe. Ukija Mtwara pale kati kulikuwa na nchi kamili ambayo mpaka
wake unaishia sehemu moja inaitwa Jiwe la mzungu kule Lindi na unaanzia
eneo fulani kule Msumbiji. Mzee mmoja alijaribu kufuatilia wakati wa Utawala
wa Mwalimu akataka kuidai hiyo nchi lakini kilichomkuta...... si mada yangu hapa
Kuhusu Tanganyika na mimi pia sijui.
 
Neno Tanga ni la Kiarabu limetokana na neno Tanja na Waarabu walipofika pwani ya Afrika mashariki ijulikanayo kwa sasa kama Tanga, waliufananisha na mji uitwao Tangier (Morocco) na kwa kuwa Tanga kulikuwa na msitu unaoingilika (Nyika) na ili kutofautisha kati ya Tanja ya mjini na Tanja ya nyikani, ikaitwa Tanganyika ikimaanisha kutofautisha baina ya Tanga (mji) na kuingia (Ushenzini) Tanga-nyikani.

Huwezi kuuondoa Uarabu uliopo Afrika, hata ufanye nini, kwani Uarabu mwingi upo Afrika kuliko huko kunakojulikana kwa sasa kama Uarabuni. Huo ndio ukweli. Amini usiamini.
 

Duuh!!!!!!!
 


Asante FaizaFoxy.
 
Thanks to all walionchangia naendelea kujifunza ingawa naona kuna mawazo tofautitofauti.
 
Kuna sehemu kati ya Muheza na Tanga katika Mkoa wa Tanga ambayo inaitwa Tanganyika inawezekana ikawa ndiyo chanzo cha jina hilo kutumika kwa nchi nzima.

Neno Tanganyika nila kibantu; na mfano kwa washona lina maana ya mahala maisha yanapoanzia. Ni vipi limekuwa jina la nchi yetu hiyo history siifahamu vizuri lakini la weza kuwa lilianza kutumika rasmi kama jina la nchi wakati wa scramble and partition for Africa ambapo ramani ya Africa ndipo ilipochorwa na mipaka ya nchi kuwekwa.
 
Hapa sipo. Historia F kichwan.
 
Hapo mi simo. History F kichwan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…