Nini cha kufanya baada ya gari kutolewa namba na kampuni iliyoteuliwa na TRA?

mpita-njia

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2010
Posts
1,734
Reaction score
1,616
Habari za Leo,

Wiki iliyopita gari yangu ilikamatwa na kampuni binafsi iliyoteuliwa na TRA kukamata magari ambayo hayajalipiwa kodi ya mapato, gari ndio kwanza imeanza kazi.

Mtu wa kampuni hiyo alifungua plate number akang'oa bima na road licence, dereva wangu akarudisha gari garage kwetu.

Wiki moja baadae nimeonda office kwa hao jamaa naambiwa nilipie shs 200,000. Wakati gari inakamtwa hakuna karatasi yoyote tukipewa wala sehemu yoyote tulisign.

Hii amount ni kubwa ukifikiria nimetoka kuwalipa TRA shs 500,000 ya kodi ya mapato.

Naomba msaada wa namna ya kufanya.
 
Sheria gani imewaruhusu kubandua bima na plate no???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…