SoC04 Nini cha kufanya ili kuboresha sekta ya afya katika miaka 5 ijayo na kuendelea

SoC04 Nini cha kufanya ili kuboresha sekta ya afya katika miaka 5 ijayo na kuendelea

Tanzania Tuitakayo competition threads

Idol Spyce

New Member
Joined
Jun 22, 2024
Posts
1
Reaction score
2
STORY OF CHANGE
NINI CHA KUFANYA ILI KUBORESHA SEKTA YA AFYA KATIKA MIAKA 5 IJAYO NA KUENDELEA

UTANGULIZI

Tanzania ya Sasa Imeendelea Katika Sekta mbalimbali Tofauti na hapo Mwanzo katika Miaka ya Nyuma Lakini Ukiilinganisha Nchi yenu na Baadhi ya Nchi kadhaa Utagundua kuwa Bado Tunahitaji Maboresho Na Maendeleo Zaidi katika Sekta Hizo.Katika Story Of Change(Soc) Ningependa Zaidi Kuongelea Sekta ya Afya,Kama Mjuavyo Kumekuwa na Changamoto Nyingi Sana katika Utelekezaji wa Huduma za Afya ,Kutokana na Changamoto Hii Kumejitokeza Vifo vya Watu Wengi Sana,Kuna Vifo vilivyojitokeza Kutokana na Mgonjwa kukosa gharama za Matibabu,Kuna Vifo Vilivyojitokeza Kutokana na Mgonjwa kushindwa kupata huduma kwa Wakati na N.k


BAADHI YA WAGONJWA KUSHINDWA KULIPIA GHARAMA ZA HOSPITAL

Tuanze na Hii Ambayo Inasababisha Vifo kwa Wagonjwa Walioshindwa gharama za Hospital ;- Kuna Baadhi ya Huduma za Kijamii katika Tanzania yetu ili Kuzipata inahitaji Utoe Pesa na hii imekuwa ni Changamoto kubwa Sana katika kaya Maskini na Kwa Wale watu Wenye Uwezo wa Chini.Kuna Baadhi ya Hospital Huwezi Kuanzishiwa Huduma yoyote Bila kutoa kiasi chochote cha Pesa na Hii imekuwa Sababu Moja wapo ya kusababisha Vifo kwa Wale watu Wenye Hali ya Chini. Ivyo Basi Inatupasa Tuweke Mipango Mikakati ili kuhakikisha Tunatokomeza Vifo Vitokanavyo na Kukosekana Kwa Gharama za Matibabu Kwa Watu Wenye Hali Duni.

Kwanza Kabisa Tuhakikishe Kila Mtanzania Anakuwa na Bima ya Afya itakayomuwezesha kupatiwa Matibabu kirahisi Mpango huu Uwekwe kuwa kila Raia ni Lazima Awe na Bima ya Afya kama ilivyokuwa katika kitambulisho Cha Uraia Hii Kidogo Itawapa Motisha Watanzania na Kuboresha Sekta ya Afya katika Miaka Mitano ijayo japokuwa Haitoondoa kabisa Tatizo hilo bali Tutakuwa Tumepiga Hatua Mojawapo ya Kupunguza Vifo Ambavyo Hutokana Na Ukosefu wa Gharama za Matibabu

Pili Tuweke Mipango Thabiti itakayomuwezesha kila Mtanzania Kulipia Bima ya Afya;-Kila Ifikapo Mwisho Wa Mwezi Watanzania Hutoa Kodi za Majengo ivyo Basi Uwekwe Mpango wa Kukusanya Malipo ya Bima kupitia Luku kama Wafanyavyo kwenye Majengo pia Serikali ifanye Makato hata ya Shilingi 200 Kwa kila Mwezi Kupitia Laini ya Simu kwa kila Mtanzania, Na Kwa wale Wasiofikisha Umri wa Miaka kumi na minane(18) Na Wasiokuwa na Simu za Mkononi Malipo yao Yafanyike kupitia Laini za Wazazi au Walezi wao.Japokuwa Haitoondoa Tatizo Bali itafanya Nchi kuendelea na kuwa Bora Zaidi katika Sekta ya Afya.

VIFO VITOKANAVYO NA KUKOSEKANA HUDUMA KWA WAKATI

Tumalize na Vifo vinavyojitokeza Kutokana Na Mgonjwa kukosa Huduma kwa Wakati;- Vifo Vingi Vimekuwa Vikijitokeza Kutokana na Baadhi ya Wagonjwa Kushindwa Kupatiwa Huduma kwa Wakati,Kuna Baadhi ya Sababu Ambazo Huchangia Ucheleweshaji wa Huduma kwa Wagonjwa na Kusababisha Vifo.

Upungufu Wa Magari ya Kubebea Wagonjwa;-Kutokana na Uchache wa Magari ya kubebea Wagonjwa kwa baadhi ya Hospital Imekuwa ni Mojawapo ya Changamoto Ambayo huibua Vifo vingi sana vya Ucheleweshaji Huduma kwa Baadhi ya Wagonjwa.

Iwapo Magari ya Kubebea Wagonjwa yangekuwa Mengi basi Ingepunguza Asilimia ya Vifo vitokanavyo na Ucheleweshaji Huduma kwa Maana yangefika Kwa Mgonjwa kwa Wakati Husika na Mgonjwa kuanza kupatiwa Huduma ya kwanza Akiwa Ndani ya Gari la Kubebea Wagonjwa na Baada ya kufika Hospital Angepewa Huduma Nyingine, Lakini Kutokana na Uchache Wake Ikatokea Wagonjwa Zaidi ya Wawili Kuhitaji Huduma ya Gari la Wagonjwa Haitowezekana Kwenda kwa Wakati kwa Wagonjwa Wote Ivyo Itaenda kubeba Baadhi ya Wagonjwa kutokana na idadi ya Gari za kubebea Wagonjwa wa Dharura(Ambulance)Ivyo Wagonjwa Wengine Itawalazimu kuchukua Usafiri Mwingine Ambao ikitokea Njiani kukawa na Foleni basi Itawalazimu Wasimame kwenye Foleni na Hii Usababisha Vifo kwa Baadhi ya Wagonjwa Maana Wanakuwa Wanakaa Barabarani Mda Mrefu Tofauti na Watakaopanda Gari la kubebea Wagonjwa Wao Hawatasubiri katika Foleni yoyote maana Magari hayo Hujulikana kama Gari la Dharura Ivyo basi Serikali ifanye Mpango Mkakati ili kuhakikisha Magari ya Kubebea Wagonjwa yanakuwa Mengi ili kuhakikisha yanawafikia Wagonjwa kwa Wakati Muafaka,Hii pia italeta Maendeleo katika Sekta ya Afya.

Lakini Pia Kitu kingine Ambacho Husababisha Vifo vya Wagonjwa Ni Upungufu wa Vituo vya Afya ;- Katika Baadhi ya Maeneo Mbalimbali Kumekuwa na Upungufu wa Vituo vya Utoaji Huduma ya Afya,Unakuta Katika Wilaya Nzima za huko Vijijini kuna Hospital Moja tu hii Upelekea Baadhi ya Wagonjwa kukosa Huduma kwa Wakati na Kupelekea Vifo,ivyo Serikali iweke Mikakati ya Kuongeza idadi za Hospital Kwa kila Wilaya kuwe na Hospital za Kutosha

Upungufu wa Wauguzi;-Hii pia Imekuwa Ni Changamoto Mojawapo Katika Sekta ya Afya,Kuna Baadhi ya Hospital Zimekuwa na idadi Ndogo ya Wauguzi na Hii hupelekea Wagonjwa Kutopata Huduma Za Matibabu kwa Wakati na Baadhi ya Wagonjwa Kufariki kutokana na kutopewa Matibabu kwa Wakati ivyo Serikali yetu Watoe Ajira Kwa Wingi Kwa Watu Wenye Elimu Ya Kitabibu Hii Itasaidia Kuboresha Sekta ya Afya lakini pia itakuwa imesaidia Kupunguza jopo la Watu Wenye Ukosefu wa Ajira Waliosomea Fani ya Kitabibu.

Ukosefu wa Baadhi ya Huduma za Vipimo na Matibabu katika baadhi ya Hospital;-Hii Imekuwa ni Mojawapo ya Changamoto kubwa Sana katika Sekta ya Afya,Ni Hospital Chache Sana Nchini Ambazo Hutoa Huduma Za Vipimo kwa Baadhi ya Magonjwa,Si Hospital Zote Nchini Hutoa Huduma ya Ultrasound pia Si Hospital Zote Hutoa Huduma za Vipimo vya Saratani ivyo basi Serikali yapasa kuhakikisha Kila Hospital inatoa Huduma Zote Za Kitabibu hii itakuwa Ni njia Mojawapo ya Kuboresha Sekta ya Afya.


HITIMISHO

Ivyo Basi Kama Serikali yetu ikizingatia Na Kuyatekeleza Yote Niliyoyasema Hapo juu Katika Miaka Mitano ijayo na kuendelea Tanzania yetu itakuwa Imeendelea sana Katika Sekta ya Afya,Ivyo Serikali ianzishe Mifumo Thabiti ya kuhakikisha kuwa Yote yaliyotajwa hapo juu yanafanyiwa kazi ili Kufikia Malengo ya Kuboresha Sekta ya Afya.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom