MAMESHO
JF-Expert Member
- Jul 5, 2011
- 1,432
- 1,738
Habari za leo. Awali niliwahi kuandika uzi kuelezea dalili zinazojitokeza ili kujua kama unatumika kwenye uhusiano.
Baada ya kukaa na kuangalia uhusiano ulionao, na kuona zile dalili unaweza kujua kuwa ni eneo gani umeathirika zaidi.
Yapo mahusiano yanaweza kuathiri akili yako, yako yanaweza kuathiri hisia zako, yapo yanaweza kukuathiri kiafya kwa maana ya mwili wako na maeneo mengine mengi.
Lengo la wengi kutumia watu wengine ni ili kuweza kukidhi hitaji lao. Kwa mfano hitaji la kimapenzi, hitaji la fedha, fursa, au kukamilisha lengo lolote walilo nalo.
Wakati mwingine wanaotumia watu wanaweza kuwa na ugonjwa wa kisaikolojia hivyo kuathiri afya yako kupitia ukatili wanaoweza kufanya. Katika jambo hili hakuna jibu la moja kwa moja. Jambo la msingi ni kutambua ni eneo gani unalotumika, hapo unaweza kutambua njia sahihi ya kujikwamua.
Moja ya namna ambayo unaweza kuitumia ni kuzuia lengo la anayekutumia lisifanikiwe, ila utaweza kugundua pale tuu ambapo utakuwa umegundua unatumika eneo gani. Ikiwa mpo kwenye mahusiano ya kudumu na mhusika, kwa mfano ndoa, unaweza kufanya tathimini ya uamuzi unaoweza kuchukua ili uwe salama.
Ngoja nikupe mfano mmoja.
Miaka mitano iliyopita rafiki yangu mmoja alikuwa nafanya kazi serikalini inayojihusisha na ukusanyaji wa mapato katika ngazi ya wilaya. Yupo mfanya biashara mmoja ambaye kila sikukuu alikuwa akimletea zawadi mbali mbali. Zawadi za vinywaji na zawadi za kuwapa watoto. Lakini alikuwa na lengo.
Kampuni yake ipatiwe makadirio nafuu. Kupitia vizawadi vya hapa napele maamuzi mazuri yaliweza kufanyika juu yake. Na alifanikiwa kwa alichokuwa anakitaka kwa muda mrefu sana. Lakini pale mhusika alipokuja kubaini aliweza kuziba mianya yote ambayo mhusika anaitumia. Haya mambo yapo kwenye kila eneo la maisha. Muwe na siku njema.