Nini cha kuzingatia kabla ya kununua mashine za EFD (mashine za TRA)

Nini cha kuzingatia kabla ya kununua mashine za EFD (mashine za TRA)

bolsto

Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
36
Reaction score
5
Habari wana Jamii,

Vitu muhimu vya kuzingatia kabla ya kwenda kununua mashine ya efd. Wengi kama binadamu wa kawaida tunaangalia zaidi bei nafuu, especially kwa mtu ambaye hanunui kwa hiyari.


  • Chagua supplier ambaye upo karibu naye au wana office yenye technician. hii ni kwa sababu ki sheria, mashine inapoharibika, inatakiwa ifikishwe ofisini ndani ya masaa 24 na kutengenezwa ndani ya masaa 48. endapo upo mbali na supplier, itakua kwako ni usumbufu sana. mara nyingi mashine sio shida ila network/server ya tra inasumbua, ila ata kama ni hivyo ni lazima u report pindi unaposhindwa kutuma z-report.

  • Pili chunguza ni mtandao gani kati ya airtel au vodacom unafanya vizuri hapo ulipo. hizi mashine zinatumia mitandao hiyo miwili kuwasiliana na server ya tra (nb: tra ndio wanalipia gharama). kwa hiyo ukifahamu hilo, unapoenda nunua mashine ni bora uwataarifu ikiwezekana wakuwekee line inayoendana na mazingira yako.


  • Ubora wa mashine. mashine zote zinazouzwa hapa Tanzania, zimethibitishwa na TRA kwa maana hiyo zote zina viwango vinavyotakiwa. ila kutokana na uzoefu wa watu, ingawaje zote ni bora, kama ilivyo vitu vingene vya electronics ila zinazidiana kwa ubora. mfano hata kwenye simu: tecno, samsung na nokia zote bora ila bei zinatofautiana. kuna mashine kama Datecs DP 25, incotex 130, HCP best LC, ni mojawapo za mashine zinazosika kwa ubora na perfomance. sema na bei zake ziko juu kidogo. uzuri ni kwamba hela yako mwisho wa siku unarudishiwa na TRA kama kodi.

Kama una swali zaidi niulize, mana humu tupo kuelimishana, mimi TRA approved technician, nafanya kazi kwenye kampuni ya Bolsto Solutions Ltd.

0758 717 754 na 0658 555 903
 
Kuna mashine zingine usipotuma z-report kesho yake unaweza kutoa risiti kama kawa ila inakupa tu notification kama yamepita masaa 48 bila kutuma ila zingine bila z-report hutoi risiti. Kwa nini kuna utofauti?
 
Mashine za phaze II zimekua na restrictions nyingi zaidi. programs na requirements za mashine zinakua defined na TRA.
Phaze I ilikua ile 2010 kwa watu wa VAT tu, hii project ilipoanza. hata hivyo ni mashine chache sana ambazo zinaweza kukuruhusu kuuza bila kutuma Z-report labda kama ni ESD. mashime zingine huwa zinatuma automatically, hata kama wewe usipo tuma. mfano mashine za HCP ukiingiza tu password kama kuna pending z itatuma yenyewe.
 
Halafu...hiyo system ya kupokea z report sio automatic I mean lazima awepo mtu anayepokea? Maana ukithubutu kuchelewa kutuma tu haiendi mpaka kesho may be saa sabaa....
 
hapana, ni automatic, ni server/computer ndio inapokea. kuchelewa kupokelewa ni network tu inakua inasumbua. sometimes server inakua down sana au overloaded. mida ya usiku na asubuhi z-report zinakua azisumbui sana kama mchana. unajua so far server iko moja tu kwa tanzania nzima.
 
Back
Top Bottom