Nini chanzo cha hili tatizo la kuondoa herufi 'h' kwenye baadhi ya maneno?

Nini chanzo cha hili tatizo la kuondoa herufi 'h' kwenye baadhi ya maneno?

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Habari zenu wandugu? Hili tatizo la baadhi ya watu kuondoa herufi 'h' kwenye maneno linazidi kukua. Kila siku nakutana na maneno haya: ataki badala ya hataki, uyu badala ya huyu, awezi badala ya hawezi nk.Bila shaka hata wewe umeshakutana na maneno ya aina hiyo. Je, watu wanafanya kwa makusudi au ni kweli wana matatizo na herufi 'h'? Chanzo chake nini?
 
Mkuu hisia zangu zinaniambia kua watu hawafanyi makusudi,nimegundua ni moja ya matatizo mengi kwenye uandishi watu wanashindwa kujua herufi ipi ikae wapi.kiswahili chetu wenyewe na kinatupiga chenga,
 
Mkuu hisia zangu zinaniambia kua watu hawafanyi makusudi,nimegundua ni moja ya matatizo mengi kwenye uandishi watu wanashindwa kujua herufi ipi ikae wapi.kiswahili chetu wenyewe na kinatupiga chenga,
Na kweli@Kukamido, wengi wanapigwa chenga kwa jinsi tatizo lilivyo kubwa!
 
Kwa maoni yangu, tatizo ni kwamba ufundishaji wa lugha nchini Tanzania haujatiliwa mkazo kabisa. Tunayona matokeo kwenye Kiingereza kirahisi zaidi. Kwenye Kiswahili sasa yanaanza kujidhihirisha. Kama ulisoma Kiswahili vizuri, lazima utafahamu kwamba "Amina ana Kitabu" ni tofauti kabisa na "Amina hana kitabu." Tena huhitaji kuwa umesoma Kiswahili mpaka kidato cha nne ili kulijua hili. Ushahidi mwingine wa jambo hili angalia hata watu wanaoandika katika forum kama hii wanandikaje. Wengi wanaandika bila mtiririko unaoeleweka. Hawatumii alama za vituo ipasavyo, hawapangi sentensi inavyotakiwa. The state of language education in Tanzania is absolutely pathetic.
 
Back
Top Bottom