Underwood
JF-Expert Member
- Dec 25, 2020
- 1,909
- 3,120
Wengi wetu tunafahamu kuwa Kenya ipo katika vuguvugu la uchaguzi mkuu utakao fanyika tarehe 9 August mwaka huu (2022).
Katika harakati hizi za uchaguzi ni wazi kuwa mchuano ni mkali kati ya kiongozi wa upinzani wa muda mrefu nchini Kenya, Raila Odinga 'Baba' na makamu wa Rais, William Ruto 'Hustler'.
William Ruto ni makamu wa Rais anaye maliza muda wake, Uhuru Kenyatta. Safari ya kisiasa kati ya hawa wawili ilishika hatamu na kupelekea kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika March 2013 ambapo kwa pamoja walishinda kinyang'anyiro cha Urais kwa asilimia 50.51% dhidi ya Raila Odinga na Kalonzo Musyoka.
[Ruto and Uhuru 2013]
Fast forward mwaka 2017 Uhuru Kenyatta na William Ruto walichaguliwa kwa mara nyingine tena baada ya uchaguzi kufanyiwa marudio kwa amri ya mahakama. Ni wazi hadi kufikia hapa bado uhusiano kati yao ulikuwa mzuri na ndiyo maana Ruto alikuwa mgombea mwenza na kisha makamu wa Rais.
[Uhuru and Ruto]
Katikati ya mwaka 2019 palianza kuzuka kwa taarifa za kuwepo kwa ufa kati ya Rais Uhuru na makamu wake William Ruto huku chanzo cha ufa kikiwa hakipo wazi sana hasa kwa wale wanao fuatilia siasa za Kenya.
Sasa ni mwaka 2022 huku uchaguzi mkuu wa Kenya ukikaribia, ufa katika uhusiano kati ya watu hawa wawili ambao hapo mwanzo walikuwa marafiki wakumbwa walio kuwa pamoja katika shida na raha (mfano kesi ya ICC) sasa umegeuka na kwa mpasuko mkubwa ambao sio rahisi kuuziba na unaonekana wazi kabisa.
Baada ya kuanza kwa harakati za uchaguzi wa mwaka 2022, Rais Uhuru Kenyatta ameonyesha mara nyingi kile kinacho itwa kumuunga mkono waziwazi mpinzani namba moja wa Ruto katika kinyang'anyiro cha Urais, Raila Odinga huku zaidi ya mara moja Kenyatta amekuwa akitoa kauli zisizo za moja kwa moja zinazo mlenga William Ruto jambo linalo dhoofisha kwa namna moja au nyingine safari ya Ruto katika kuusaka urais.
Tanzania tumewahi kuona/kuhisi ufa kati ya pande mbili wakati wa safari ya kuutafuta urais baina ya miamba mbalimbali ya siasa lakini sio mashambulizi ya waziwazi baina yao.
[Uhuru and Ruto]
Swali langu (na kwa niaba ya wengi):
NINI CHANZO CHA MPASUKO HUU HADI KUPELEKEA UHURU KENYATTA KUMPIGA VITA WAZI WAZI (ALIYEWAHI KUWA) RAFIKIYE WILLIAM RUTO?
Karibuni, nawasilisha.