Mkuu Nansawa,
Premature rupture of membrane(PROM), ni tatizo ambalo hutokea (Mfuko/Chupa kupasuka) angalau masaa 12 na zaidi kabla ya uchungu tayari kwa kujifungua(labor).
Ingawa bado kuna tafiti nyingine zinazoendelea, sababu kubwa hasa ni udhaifu wa mfuko/chupa(generalized weakness of the amnion, chorion) pamoja na severe/excessive contraction za tumbo/mfuko wa uzazi.
Mambo kadhaa yanaweza/yamehusianishwa na tatitzo hili (PROM) yakiwepo uvutaji wa sigara, infections wakati wa ujauzito, matibabu ya baadhi ya magonjwa(mf.saratani ya shingo ya uzazi), matatizo ya Connective tissues, historia ya kuwa na tatizo hili n.k.
Ni vizuri, kwa mwanamke kuwahi hospitali kwa ajili ya uchunguzi agunduapo hili, hii itasaidia katika kumkinga mama(mjamzito) na mtoto wake na maambukizi, lakini pia kuokoa maisha ya mtoto.