Nini chanzo cha wanawake na watoto wa DSM kupenda chips mayai kuliko vyakula vingine?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Wanaume sio sana, ila kwa utafiti wangu wanawake, Wanafunzi na watoto wadogo wa kike na wa kiume wanapenda chakula hiki kuliko kitu chochote.

Tena cha ajabu hata wakipikiwa nyumbani wanasema za nyumbani sio tamu.

Cha ajabu zaidi hata uwatoe watu mikoani waliozoea ugali wa udaga au mtama ndani ya mwezi tu na wao wanakuwa wahanga wa chakula hicho.

Chanzo ni nini?

Ilitokeaje hiki chakula kikawa na nguvu kubwa kiasi hiki au ni dunia nzima kwenye miji mikubwa hali huwa hivyo?

Ni hayo tu.
 
mkuu mbona hata huku mikoani wanapenda?

ndo chakula chao mkuu

nadharia yangu ni kwamba, kwavile chipsi zinanenepesha, na mtazamo wa wengi ni kwamba wanaume wanatakiwa wawe wakakamavu sio wanene, basi chipsi zikaonekana zinawafaa zaidi wanawake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…