lugamba2001
Member
- Aug 18, 2009
- 12
- 0
Ndugu wana jamii forums! hoja yangu, ni nyepesi kuisoma lakini ukiiangalia kwa undani ni nzito! najua kila mtu aweza kutoa jibu lake kwa haraka haraka, lakini mimi napenda tufikirie na tutafiti kwa umakini mkubwa na pengine waliokwishafanya utafiti watuambie, labda tunaweza kuioko jamii yetu!
Mojawapo ya mambo yaliyonishangaza toka nifike India miezi kadhaa iliyopita, ni kukosekana kwa matukio ya wizi! Licha ya umaskini uliokithiri miongoni mwa vijana wengi katika nchi hii, ikiwa ni pamoja na tatizo la ombaomba na wazee na watoto wa mitaani! Kila ukipita katika majiji makubwa ya nchi hii utakuta watu wengi sana wakifanya biashara za "kimachinga", vibarua na wakilala pembezoni mwa majengo makubwa au kwenye vibanda, kama vile vya kulindia nyani wasile mahindi kule Kasulu vijijini. lakini hawa wanaishi kwenye majiji, kuna magari, pikipiki na baiskeli zisizo na idadi... l
Jambo moja tofauti na Bongo ni kuwa, hawatakukaba na kukuibia simu, wala hawatakuchomoa pochi yako mfukoni au kukuuzia simu feki achilia mbali roba ya ubao wakikutana nawe gizani au penye kichaka! Mashirika ya umma ndiyo yanafanya biashara zote muhimu za nchi wala hayajafirisika hata wakati mmoja. Sasa swali kwa nini bongo? ukiuliza watakuambia hali ngumu ya maisha? yaani umaskini! ni kweli? mbona wahindi wana hali ngumu? naweza kusema, hata zaidi na bado hawaibi? kuna nini nyuma ya wizi wa Bongo? jamani nisaidieni!