Nini chanzo, na tiba ya shingo ya kuku kupinda kuelekea kishoto au kulia kusiko kawaida?

Nini chanzo, na tiba ya shingo ya kuku kupinda kuelekea kishoto au kulia kusiko kawaida?

Inaweza ikawa upungufu wa Vitamin E au Ugonjwa wa Coccidiosis,mabawa yao yapo kawaida au yameshuka ? Wanaharisha ?
 
Inaweza ikawa upungufu wa Vitamin E au Ugonjwa wa Coccidiosis,mabawa yao yapo kawaida au yameshuka ? Wanaharisha ?
Mabawa hayajashuka na wala hawaharishi isipokuwa shingo zinapinda, wanashindwa kula, kutembea kawaida na hata kulala, wanalala mithiri ya mtu alilala ubavu.

Kwa nyongeza kuna mwingine shingo haijapinda ila yuko kama kapooza miguu na hawezi kutembea kabisa inaelekea mwezi na nusu sasa. Kula anakula vizuri tu.
 
Mabawa hayajashuka na wala hawaharishi isipokuwa shingo zinapinda, wanashindwa kula, kutembea kawaida na hata kulala, wanalala mithiri ya mtu alilala ubavu...

Hiyo inaonekana itakuwa upungufu wa Vitamin E, huyo anayeweza kula angalau mpe zile dagaa kwa ajili ya chakula cha kuku huwa zinaongeza vitamin, kuna jamaa niliwahi kusikia anawalisha supplement inaitwa Amintotal pia, ila jaribu kuangalia chakula unachowapa kwa umakini
 
Unawafugia ndani au wanajitaftia chakula?
Nilikuwa nawafungia ndani toka watotolewe hadi walipofikisha miezi mitatu hivi.
Kwa sasa wana miezi miwili tangu niwaachie na tatizo limejitokeza ndani ya miezi hii tangu niwaachie.
 
Nilikuwa nawafungia ndani toka watotolewe hadi walipofikisha miezi mitatu hivi.
Kwa sasa wana miezi miwili tangu niwaachie na tatizo limejitokeza ndani ya miezi hii tangu niwaachie.
Kuna uwezeKano wakawa wnasumbuliwa na ukosefu wa Vitamin/Madini. Nenda Vet shop ya karibu ukawataftie solution
 
Wa kienyeji.
Hiyo kitaalam wanaita neck twisting

Huwapata Mara nyingi kuku wanaofugwa ndani

Chanzo Ni ukosefu wa vitamin E au selenium

Chakufanya.. nunua multivitamin kutoka duka la mifugo changanya katika maji Yao safi ya kunywa pia walishe mboga za majani

Wale kuku wanaoshindwa kula walishe mwenyewe

Nb tatizo hili husababishwa pia na magonjwa mengine hasa pale wanapokuwa hawajapata chanjo Kama newscastle

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom