JokaKuu,
Mkuu nazungumza yote haya kutokana na experience sio habari ya kusimuliwa.
Kifupi najua wengi wenu miaka hiyo mlikuwa shule iwe Chuo kikuu ama sekondari lakini mimi nilikuwa tayari mitaani nikibangaiza.
Nakwambia hapakuwa na Ubaha wakitu chochote ktk uzalishaji isipokuwa vitu vyote hivi vilizalishwa kwa minajiri ya biashara ya ndani kutosheleza mahitaji yetu..Unapozungumzia swala la Bia nakumbuka vizuri Breweries walikuwa na matawi hadi vijijini na kuna jamaa mmoja Mganda akiitwa Peter alikuwa mlanguzi mkubwa wa bia hizi kuzipeleka Uganda.
Miaka hiyo usafiri wa meli za abiria na mizigo ulikuwa ulikuwa ukienda Uganda na Kenya kila week mara tatu na mizigo minmgi ilikuwa bidhaa zetu wenyewe. Huku kusini Mbeya pia vijana walichemka kupitisha mali kwenda Zambia na ni wakati huo nimekaa sana Mbeya mjini na kuja fahamiana na vijana wa Mbeya ambao nilikuja kuwa mwenyeji wao mjini wakikaa pale Hotel Continental..Najua watashangaa sana kusikia mimi ndio Mkandara yule mhuni wa Holiday.
Hivi wewe unafikiria wale machinga wa Kichagga wenye mabanda ya michubuo na madawa ya nywele waliweza vipi kuyaingiza nchini wakati mgumu kama ule...Mkuu, Uhaba ulitokea kwa sababu mali nyingi zilisafirishwa nje, fedha ya kigeni kwetu ilikuwa shilingi ya Kenya..Dollar ilikuwa haipatikani benki kuu hivyo kuuza mali zetu nje ndio njia pekee ya watu kukusanya dollar bila kupitia benki kuu na wahindi ambao walikuwa wateja wakubwa wa dollar..Nitarudia kusema ni maisha ambayo nimeyapitia na nafahamu kwa upana zaidi ya haya nayoandika hapa..
Sema tu ktk operation hiyo walidhurika wengi.. Askari wetu badala ya ku target sehemu zinazotakiwa walianza kufanya wao biashara ya mshiko. Ukikutwa na kifuko tu unasimamishwa na kuulizwa umebeba nini.. Ikiwa mali wanachukua na utarushwa kichura kwa chupi moja ya toka mtoni. Ikafikia kwamba tulikuwa tumepoteza maana ya vita ile na kuwa kila mwanancvhi ni mkisiwa wa Uhujumu.
Kuna marafiki zangu wakija Mbowe na kutanua enzi hizo kutokana na uuzaji wa sigara, Khanga za Urafiki, zana za Ufi, Besco, Gafco, Bima na kadhalika wote walikuwa wakitanua kwa uuzaji wa mali na ma deal ya serikali kwa walanguzi chini ya meza na sio kwa minajiri ya kuwafikia wananchi bali kusafirisha nje kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumshika mtu na mali hizo.
Ziwa victoria lilikuwa uwanja wa mapambano na ni katika wakati huo jeshi letu liliweka meli za kivita kufukuzia makalua yaliyojaa mali..Mkuu vijana wote miaka hiyo tumeishi kwa kubangaiza, Ukame ulikuwepo lakini hata siku moja sikuwahi kupanga jiwe dukani kwa mhindi tulijua wapi mali inapatikana. Tulijimwaga Mermaid na Salamander kila siku kama vile hakuna shida na jambo moja muhimu sana la kujiuliza wewe ni hili..
Kwa nini pamoja na Ukame wote ule kuna bar zilikuwa hazikosi Pombe..Hata siku moja tulipokuwa disco sio Mbowe, Africana, New Afrika, Vision, Silversand, Rungwe na sehemu kibao hatukuwahi kuona ukosefu wa bia hizo! wala kusikia kwamba Breweries walishindwa ku supply. Kuna hotels ambazo kila siku zilikuwa na chakula kama kawaida tena kwa bei nafuu ajabu. Lini ulikwenda Azam ukakosa Pilau na Biriani! Au Mermeid ukakosa Chips..
Nakumbuka wakati mmoja nikienda Uganda kwa hayo makalua ilibidi tutupe magunia ya sukari kupunguza uzito kwani kalua lilikuwa likiingiza maji...Na kibaya zaidi basi walanguzi wote waliokuwa wakichukua mali hizo adimu walirudi nchini na Mitumba, vipodozi na mashati ya Juliana toka toka Dubai..
Kwa hiyo tatizo la nguo, vipodozi, sabuni, dawa za miswaki nchini ilikuja sababisha uhaba wa vitu muhimu sana kama chakula..kwa ubadilishaji wa mali kwa njia haramu na wakati huo huo supply kutoweza kutosheleza demand.
Kila Nyerere alijaribu kuweka ngumu ktk kuhakikisha bei nafuu kwa wananchi ndio kwanza wafanya biashara walificha mali hizo. Demand iko palepale na supply ikaonekana hakuna.. Nakumbuka maduka mengi waliweza kuuza asilimia 20 ya stock yao na kudai kwamba mali imekwisha.. usiku wanakuja walanguzi na kupewa mali iliyobakia kwa bei ya juu zaidi ya ile ya serikali, hivyo price control pia iilichangia sana..Mkuu yote haya nazungumza kiuchumi na economics inakubali kabisa sababu nilizoziweka hapa.. It's the fact sio najaribu kutumia kitabu kama wasomi wengi wanavyotaka watu kuamini kuwa uchumi wetu ulianguka kutokana na Ujamaa peke yake.
Kweli kabisa Ujamaa ulichangia sehemu kubwa kwani mashirika yote yaliyokuwa yakizalisha mali nchini yalikuwa hayawezi kujiendesha zaidi ya kutegemea bajeti ya serikali. Kama yangepata mfumo fulani wa biashara biashara na somehow kama China ya leo, yakawa private with some regulation and govt control in policies za responsibility kwa viongozi wake, yakaweza kujiendasha yenyewe labda pengine tungeweza kutokana na tatizo la Uhaba wa vitu.
Kama nilivyosema hapo awali mwalimu Nyerere alishindwa kuziba tobo za Uhujumu uchumi ktk Ujamaa kwa sababu hakufahamu shina la Uhujumu uchumi lilitokana na watu aliowaweka madarakani kuendesha mashirka hayo.. Muulize hata FMES atakwambia viongozi wetu wa leo ktk serikali ndio wale wale waliokuwa viongozi ktk mashirika ya Umma na ndio wao waliotufikisha hapa tulipo. Ndio mafisadi wakubwa wa Ujamaa wenyewe walioiba na kufilisi mashirika hayo..Mtindo wa kuziba tobo haukulenga wahujumu isipokuwa mabangusilo na samaki wadogo. ukweli ni kwamba mashirika ya Umma yalikufa kutokana na viongozi wake ambao kwa wakati ule ndio walikuwa matajiri wetu.
Kitu kimoja tu ambacho namsifia mwalimu ni kwamba hata baada ya kushindwa kwake na Ujamaa lakini siku zote hakuisha kutukumbusha na kusisitiza kwamba Corruption ndio UFA mkubwa wa maendeleo yetu na tusipoweza kuziba Ufa huo basi tutakuja jenga nyumba nzima. Mwinyi hakuweza kuziba ufa zaidi ya kuweka fanicha mpya ambazo hazikuwa na faida kwetu ila mapambo ya nyumba.
Mkapa hakuweza kuziba Ufa zaidi ya kutuletea wezi wengine ndani ya nyumba yetu...Ufa umepanuka zaidi na nyumba inaanza kuingiza maji ya mvua ambayo kimazingira yetu mvua ni neema...Hiyo hiyo mvua itakuja kuwa Tsunami na hatutaweza kuokolewa kirahisi.
Uhujumu uchumi unatakiwa kupigwa vita kwa nguvu zote pamoja na kwamba ni crime ambayo haiwezi kwisha. Tukumbuke tu kwamba hujuma za uchumi nchini leo hii tunakula hata mbegu za uchumi wenyewe. Mbegu zikija kwisha nadhani tanzania itakuwa sehemu mbaya zaidi kuliko wakati wa Mwalimu.