Nini faida na hasara ya kujenga kipindi cha mvua?

Nini faida na hasara ya kujenga kipindi cha mvua?

SuperImpressor

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
1,505
Reaction score
648
Kama tunavyojua, mwaka una majira tofauti, na hivyo iwe kiangazi, kipupwe, vuli au masika, watu huwa tunaendelea kuchapa kazi ili mkono ufike kinywani.

Sasa swali langu ni kama hivyo linavyosomeka hapo juu.

Ila mimi binafsi napenda sana ujenzi wa nyumba ufanyike wakati wa kipindi cha mvua ambayo si nyingi ili ubaridi wa kipindi hicho usaidie cement iliyotumika kujengea iwe imara sana kuliko cement iliyojengewa wakati wa jua kwa sabababu inalazimishwa kukauka kabla ya muda wake.

Naomba kujua kama mawazo yangu hayo yako sawa au si sawa.

Sent from my cupboard using mug
 
Nadhani kuna faidi katk nyumba kujishindilia vzr , hasara inawez kuw kuharbka kwa cement kama mvua itawah na kuharb mbao wakat wa kuweka kenchi.
 
Vizuri zaidi vuli zinapoanza kuishia.
Unaliachia pagale lipigwe mvua, halafu likaushwe na jua.
Mvua zikiisha kabisa unaweka magrill na kuanza kupaua. Vizuri zaidi pagale liwe na mkeka kabisa.
 
Halafu ndo ukute mfuko wako umetulia na ratio wameweka kali nadhani hapo litakuwa jiwe aisee.


Sent from my cupboard using mug
 
Hata mimi napenda kujenga kipindi chenye mvua kidogo ,natarajia kuanza ujenzi hivi karibuni nianze msingi hadi lenta ila sina uhakika kipindi cha mvua kidogo ni kipi? Ushauri wadau je ni mwezi wa 12 au wa kwanza isifike mwezi wa 2?
 
Back
Top Bottom