Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Pia, wapo, hasa watu toka Bara, kuwa Zanzibar inapendelewa. Wanadhani ilipaswa kuwa kama si wilaya basi mkoa wa Tanzania.
Hawa ni wale wanaotaka serikali moja ambayo kimsingi, si chaguo la watawala. Hivi karibuni baada ya rais Samia S Hassan'kuuza' bandari ya Dar kama wengi wanavyosema, hisia na malalamiko juu ya muungano yamepamba moto. Wapo wanaosema eti wanaouza bandari wote ni Wazanzibari jambo ambalo kidogo si kweli. Kwani, kama bugne litaridhia, nalo litakuwa la wazanzibari?
Bila kuchelewesha mada na kupoteza muda, naomba tujadiliane madhara ya kukaa na muungano au kuuvunjilia mbali ili kila nchi ichukue hamsini zake. Naomba kutoa hoja.