Matatizo ya siku zote za muungano kwa maoni yangu yanaweza kupunguzwa kwa njia mbili tu,
inayotekelezeka na isiyotekelezeka. Njia hizo ni (1) kuunda serikali moja tu (SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - SJMT), yaani SMZ ielee (
be in suspense) kama inavyoelea TANGANYIKA; na (2) kuwa na serikali tatu: SMZ, SJMT na ST(SERIKALI YA TANGANYIKA). Njia ya kwanza ya kuwa na serikali MOJA, SJMT pekee, haitekelezeki bila ya kuingia gharama ambazo hazilipiki. NTAELEZA japo kidogo.
ZANZIBAR kwa sasa kiuhalisia ni nchi (dola/
state) kamili kabisa. Na hapa naomba nieleweke kuwa nimesema 'kiuhalisia' ZANZIBAR is a state, japo kisheria ZNZ is not a state (tazama hukumu ya MAHAKAMA YA RUFANI TANZANIA kati ya MACHANO KHAMIS ALLY & OTHERS V SMZ, kesi ya uhaini ya akina MAALIMU SEIF). Swali ni je, kwa nini ZNZ is a dola? KWA SABABU (1) wananchi wa ZNZ wanaamini kuwa ZNZ ni dola na taifa huru. Kwa kuwa ZNZ NI TAIFA HURU UKITAKA KUIFUTA zitaibuka vurugu ambazo gharama zake hazilipiki ; na (2) ZNZ ni dola kwa kuwa SJMT imeiruhusu itende kama dola kamili, matendo ya ZNZ ni ya kidola. Japokuwa kwa Katiba ya JMT RAIS wa ZNZ hadhi yake ni waziri katika SJMT, AMERUHUSIWA atende kama mkuu wa dola kwa (a) kupigiwa mizinga, (b) kutoa amri kwa mawaziri wenzake wa SJMT, (C) KUPEWA ULINZI wa RAIS wa dola kamili nk.
Kwa nini TANGANYIKA inadaiwa irudi? KWA sababu, kwa maoni yangu, (1) ZNZ imekuwa dola ndani ya dola JMT kinyume na inavyotakiwa iwe; (2)
kukosekana kwa mipaka inayoonekana wazi kati ya mamlaka ya SMZ na SJMT, ambapo sasa inaonekana kama vile JMT inaongozwa marais wawili na makamu wa rais watatu na mawaziri wakuu 2 nk. Kuthibitisha hayo, fuatilia matamko au maagizo yanayotolewa na viongozi kutoka ZNZ, tena kwa mambo ambayo si ya muungano, kwa watu wa TANGANYIKA na viongozi wao. HAPA HASIRA ZINAPANDA, na sauti ya madai ya TANGANYIKA inapazwa: na (3) kwa kuwa TANGANYIKA haijawahi kufa, ipo inaelea majukumu yake yakiwa yanatekelezwa na SJMT (TAZAMA KATIBA ya JMT IBARA ZA 4, 64 nk). KWA HIYO NI SUALA LA KUSEMA SASA, TANGANYIKA RUDI KAZINI.
FAIDA ZA KURUDISHWA kwa TANGANYIKA ni (1) kuondoa mikanganyiko ya kimamlaka kati ya SMZ na SJMT, kwa TANG kutekeleza mambo yanayoihusu yasiyo ya muungano kama inavyofanya sasa hivi SMZ kwa upande wa ZNZ, na hivyo kupunguza kama siyo kuondoa kero za muungano; (2) HAKI ya TANG kuishi kwa mujibu wa mkataba wa MUUNGANO kati ZNZ na TANG wa 1964; (3) kupunguza muzigo wa TANG inayoelea kuendesha shughuli za JMT, kwani TANG ikirudi basi kwa nia ya kuleta usawa ZNZ na TANG zitachangia kwa usawa kuendesha SJMT, kama ambavyo MCHANGO wa BURUNDI katika Jumuia ya AFRIKA MASH (JAM) unavyolingana na ule wa Kenya na Tanzania, na ndiyo maana BURUNDI inapewa haki sawa na nchi hizo katika JAM. Kwa sasa ZNZ inadai usawa kutoka JMT wakati haichaingii kitu chochote katika kuiendesha, wanafanya JMT inayogharimiwa na TANG kama sehemu ya kuja kuchuma vyeo, mishahara minene pasipo wao kuchangia katika MFUKO WA PAMOJA WA FEDHA WA KUENDESHA JMT; na (4) muhimu zaidi, TANG nayo kupanga mikakati yake ya kuendesha shughuli za maendeleo ya watu wake.
HOJA za kuwa MWL JKN alisema (1) kurudishwa kwa TANG ni sawa na (2) kuvunja muungano hazina mashiko. KWANZA JKN mwenyewe hakueleza ni kwa namna gani TANG ikija MUUNGANO utavunjwa. PILI hata kama alichosema MWL kina chembe za ukweli, ambazo kwa bahati mbaya mimi sizioni, MWL hakuwa MOHAMED wala YESU kwamba alichosema hakibadiliki daima. I humbly submit, part of my considered opinion ...
Humu JF kumekuwa na washabiki wa kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika ,ndani ya Muungano lakini ukiwauliza juu ya faida za kuwa na Serikali hiyo huingia mitini! Wao wanachotaka tu ni "Serikali ya Tanganyika," basi! Hawataki kusikia neno "Tanzania Bara" au vinginevyo. Pia hawajali kwamba kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika kutatimiza utabiri wa Baba wa Taifa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere kwamba kutaua Muungano kwa kuwa "Mafahali wawili hawakai zizi moja!"
Mimi napenda nifahamu "faida" na "hasara?" za kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika, kama zipo!
1. Je, ufisadi ulioishinda Serikali ya Tanzania, sasa "mbabe" wake atakuwa Serikali ya Tanganyika?
2. Je, umaskini ulioishinda Serikali ya Tanzania, Tanganyika ndiye atakayekuwa "mkombozi" wetu?
Kwa ujumla nafuu ni ipi hasa? Au tunataka kuwa kama Waisraeli walivyotaka kuwa na mfalme walielezwa hasara zake (1Sam. 8:11-20) wao walidai tu kwamba "tunataka kuwa na mfalme ili tufanane na mataifa mengine?" Je, hapa tunataka "tufanane tu na Zanzibar" kwa kuwa wana Rais wao, bendera, wimbo wa Taifa, nk? Only that?