Nini hasa hupelekea kutokujipenda baada ya kuzaa?

Nini hasa hupelekea kutokujipenda baada ya kuzaa?

MImawhite

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2017
Posts
237
Reaction score
398
Hivi inakuaje mpaka binti wa miaka ishirini kisa ndoa/au umezaa watoto wawili watatu unakuwa kama bibi wa miaka hamsini ndio majukumu au nini hii.

Maana kuna binti hapa mtaani kwetu alikuwa sister du sio wa nchi hii mrembo haswaa sasa huyu binti now amezaa watoto wawili lakini hali yake kimwili inahuzunisha hajijali tena wala kujithamini kama zamani

Akiamka na kanga aliyovaa asubuhi atashinda nayo mpaka jioni na anaona kawaida sana sasa najiuliza kilichombadilisha hasa majukumu mengi,ndio amezaa amezeeka au ndiobmaisha magumu mpaka mtu unashindwa kujipenda mwenyewe
 
Inategemea na mume alie naye,kama hajipendi asitegemee muujiza,men plays a big role on this.
 
Ameridhika na kuzaa kashazalishwa anaona hata akipendeza what for, ni perception mbaya kwakweli, Mume nae anayevumilia hii ana moyo, mimi siwezi
 
Aisee labda ni huyo tu uliyemuona
 
Hiyo ipo kwa wanaolea watoto kikamilifu yani unakuta mtu hana msaidizi na anafata kanuni za uleaji so most of the time anakua busy,kulea ni kazi wengi ambao wanakua na muda hata wa kujipodoa wanakua na wasaidizi au wanalipua katika malezi ndo maana wengine unakuta kajipodoa ila mtoto kinyaa kumuangalia yuko vuu..so mara nyingi inakua hivo mawazo na akili zote zipo katika malezi ya mtoto.
 
Na mwingine unakuta awaze kutafuta awaze kumuhudumia mtoto halafu hakuna msaidizi so muda wote yeye busy na changanya na stress za malezi basi zinabadili kabisa muonekano wa binti totally
 
Back
Top Bottom