Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Maisha ni safari ndefu yenye kila aina ya changamoto, na hakuna mwanadamu yeyote azaliwaye kwenye sura ya dunia hii bila kuzipitia. Changamoto huja kwa nyuso tofauti-tofauti kwa kila mmoja, na kamwe haziwezi kufanana wala kuwa na uzito wa aina ile ile kwa watu wote wanaozipitia.
Ikitegemea na hali, eneo, nyutu za watu, na mambo yanayowazunguka, sikuzote changamoto huwepo ndani ya maisha ya mtu kumsukuma awe na nia ya kupambana ili kujitoa ndani ya hizo na kuwa na maisha bora.
Tunaambiwa elimu ndiyo ufunguo wa maisha bora lakini hata watu wenye elimu ya juu bado huhangaishwa na matatizo mengi yanayowakosesha amani. Kila mtu mmoja mmoja anatamani kufikia sehemu nzuri maishani kiasi kwamba hata wale waliozifikia sehemu hizo bado wanakuwa hawaridhiki.
Ni tamaa yetu sote kuishi maisha yenye kuridhisha, lakini mivurugo ya maisha sikuzote huturudisha nyuma. Iwe ni kwa matajiri, au wenye hali za chini kiuchumi.
Kwa sababu ndivyo ambavyo sisi sote tumezaliwa na kukuta hali zikiwa namna hiyo tokea mwanaume wa kwanza alipoamua kumtandika ndugu yake mpaka akafa, imetubidi tuyaishi maisha kwa namna ambavyo yametutaka tuyaishi. Usione mtu anafanya jambo fulani ambalo linapingana na uasili wa kufanya mambo ukadhani hafai. La.
Ni kwamba maisha ndiyo yamemfanya akaona kufanya jambo hilo kuwa sahihi. Analazimika kuishi kwa njia hiyo aidha kwa kupenda ama kusukumwa tu, maadamu aishi.
Hivyo kamwe huwezi kuhukumu maisha ya mtu kwa kumtazama tu bila kujua kiundani ni mambo yapi yaliyopelekea mpaka akafikia hatua za kuishi namna aishivyo. Kujenga taswira nzuri mbele ya jamii ni jambo la muhimu, lakini maisha yanapokulazimu kuishi kwa namna ambayo jamii itayahukumu vibaya, unachopaswa kufanya ni kula ugali wako na kuvuta shuka kulala, ili kesho uamkie mambo mengine na kuendelea kuishi. Basi!
Naandika haya mimi siyo chizi. Mimi siyo mtunga mashairi wala nini. Ila nimeona tu nijaribu kuzama zaidi ndani ya vina virefu visivyoelezeka kwa mapana sana kuhusu neno hili: maisha. Maisha hayawezi kufanana kwa kila mmoja. Hayawezi kuendana. Hayawezi kuingiliana kwa asilimia zote na kumfanya mtu wa hali ya chini aweze kuwa kama kiongozi wa nchi hii kwa ufanisi aupatao kutokana na jasho la huyo huyo "mtu wa hali ya chini."
Kila mtu ana kisa chake mwenyewe cha maisha. Alipo fulani sasa hakufika kwa muujiza, kuna sehemu amepita. Unaweza ukashangaa kwa nini watu wanahangaika sana kufatilia maisha ya watu maarufu zaidi. Ni kwa sababu tayari wameshajijengea umaarufu.
Hawakuzaliwa nao, waliutafuta, wakaupata. Wanaoendelea kuwafuatilia tu wanaishia kuwa watu wa kutamani. Hata hao watu maarufu wamepitia changamoto nyingi maishani, lakini hakuna mtu hata mmoja aliyejisumbua kuzijua wala kuziulizia mpaka walipokuja kupata huo ufanisi na kuzigeuza changamoto hizo ziwe kitu cha kuwatia moyo wengine kupambana zaidi.
Hutajali saana kufatilia maisha ya ndani zaidi ya mwanamke abebaye sinia la karanga kichwani, akiwa amebeba mtoto mdogo mgongoni, sura yake ikiwa imechoka, akiziuza karanga hizo stendi ya mabasi na jua likiwa kali sana. Tayari tu una kitu ndani yako kinachojua kwamba ana changamoto zake, kama watu wote, kwa hiyo nawe utabaki kutulia na za kwako tu, si ndiyo? Angalau nunua hata hizo karanga basi, hata ya mia tu.
Itampa faraja kuona kwamba hata kesho anaweza kujikwamua na kuendelea kupambana kuzivuka changamoto zake ili ajenge maisha mazuri kwa kiwango ambacho Mungu atambarikia kukipata.
Sina lengo la kuandika mahubiri ili muanze kutenga sura na mistari. Ni kwamba tu nimeangalia hata maisha yangu mwenyewe na kugundua kwamba kuna changamoto nyingi zilizo ngumu maishani mwa mwanadamu, na japo kwa wengi zinatofautiana, mapenzi ni suala lizushalo changamoto kwa KILA MTU.
Kubali, kataa. Hakuna mtu apitaye upeo wa ujana bila kukumbwa na changamoto za jambo hilo. Kwa nini?
Kwa sababu hakuna lengo lolote la kuishi isipokuwa upendo. Ni kitu cha kiasili. Kila mtu anacho. Nazungumzia upendo wote, iwe ni wa kindugu, kirafiki, kishkaji, kihuni, vyovyote vile, ni lazima tu kuwe na changamoto nyingi sana. Sasa inapofikia kwenye ule upendo wa kijinsia ndiyo kabisaa! Watu mpaka wanauana kwa sababu ya kuumizwa na mapenzi.
Lakini kwa jinsi ambavyo mambo yamekuwa kufikia kipindi hiki, imeshaonekana kuwa jambo la kawaida sana kwa mapenzi kuwa kitu chenye kuumiza badala ya kutakiwa KUBAKI kuwa kitu chenye kuridhisha. Na kama nilivyosema mwanzoni, kwa sababu tumezaliwa na kuyakuta namna hiyo, basi ndiyo tunaendelea kuyaishi namna hiyo hiyo tu. Lakini kuyaishi namna hiyo hiyo tu si jambo linalofaa.
Ni muhimu kuishi kwa kusudi, na imenichukua visa vingi vilivyotokea katika maisha yangu mpaka kufikia sasa kutambua kwamba mapenzi ya kujifurahisha tu hayana faida yoyote. Yanapaswa kuwa na lengo.
Lakini kwa wengi, hata MIMI, hutuchukua muda mrefu mpaka kuja kumpata mtu anayeweza kukufanya ulitamani sana lengo hilo, haijalishi ni changamoto za aina gani utakazopitia, maadamu akiwa na wewe, unajua yote unaweza kuyashinda.
Credit: Elton Tonny