Mkaa Mweupe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 654
- 183
Waungwana naomba niilete hoja hii hapa jamvini ili tupate kuijadili.
Nimekuwa nikiwaza kwa muda mrefu sana juu ya kwanini haswa namba tatu (3). Kwani hii namba imekuwa na umaarufu wa pekee kati ya namba nyingine zilizosalia yaani 0, 1, 2,..., 4, 5, 6, 7, 8, 9.
Nianzie huu umaarufu wa namba tatu kwenye mahesabu.
Umaarufu huu haukuishia kwenye hesabu, unaendelea kwenye nyanja nyingine
Naomba kuwasilisha

- Wataalam wanatuambia ya kwamba tunaweka koma baada ya tarakimu tatu. mfano elfu moja = 1,000; elfu kumi = 10,000; laki moja = 100,000; bilioni moja = 1,000,000,000 n.k.
- Hawa wataalamu wanatueleza ya kwamba, umbo ambalo ni imara zaidi ni pembe tatu, ndio maana mapaa mengi huwa na umbo hilo.
Umaarufu huu haukuishia kwenye hesabu, unaendelea kwenye nyanja nyingine
- Hamna mgonjwa aliyewahi pewa dawa yenye dozi zaidi ya kutwa mara tatu.
- Kila mtu anatakiwa kujitambulisha kwa majina matatu.
- Waamini fulani wanaamini kuwa Mungu ana nafsi tatu.
- Wakati wa mateso ya Yesu, alianguka mara tatu.
- Yesu alisulubiwa na watu wengine wawili na hiyo kufanya idadi ya waliosulubiwa kuwa ni watatu.
- Imani hii inaendelea kwamba alifufuka siku ya tatu ilivyoandikwa.
- Jiko imara lina mawe au maegemeo matatu; angalia hata jiko la mchina na la gesi.
- Kabla ya kuanza riadha inahesabiwa moja mpaka tatu.
- Katika mashindano wanaong'ara ni mshindi wa kwanza, wapili na watatu.
- Waamini wengine kabla ya ibada lazima wajisafishe mara tatu.
- Mambo makuu kwa kila kiumbe hai ni kula kuny... na kulala.
Naomba kuwasilisha
Last edited: