Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,319
Hawa ni wale waliofukuzwa Chuo Kikuu cha Kata ya Ubungo, kutokana na kufunguliwa mashtaka na Jamhuri kufuatia mgomo wa tar 11 Novemba 2011.
Majuzi nilionana na wawili kati yao, wakaniambia kuwa kuna michakato ya kisheria wanaifanya kupinga kufukuzwa kwao kwa hisani ya Prof. Shivji, na kwa upande wa mahakamani, kesi yao ilitakiwa kusikizwa Jumanne ya tar. 20 Desemba 2011. Kutokana na mvua kubwa ya mafuriko, nikashindwa kufika Kisutu Magistrate hiyo saa mbili ilivyotakiwa, jitihada zangu zote za kusaka habari za kesi yao mtandaoni na kwenye magazeti zikakwama, kuwaona uso kwa macho ikashindikana kwa kuwa hawako tena shuleni, achilia mbali uwezekano wa kufutiwa dhamana waliyowekewa na ex-co-student wenzao wa UDSM, kwani sheria ndogo za chuo haziruhusu mwanafunzi kumdhamini raia kwa mgongo wa Afisi ya Mshauri wa Wanafunzi.
Kwa yeyote mwenye taarifa za mwendelezo wa kesi yao anifahamishe...
Natanguliza shukurani.