Nini hatima ya wanafunzi 41 waliofukuzwa shule Chuo Cha Taifa?

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Hawa ni wale waliofukuzwa Chuo Kikuu cha Kata ya Ubungo, kutokana na kufunguliwa mashtaka na Jamhuri kufuatia mgomo wa tar 11 Novemba 2011.
Majuzi nilionana na wawili kati yao, wakaniambia kuwa kuna michakato ya kisheria wanaifanya kupinga kufukuzwa kwao kwa hisani ya Prof. Shivji, na kwa upande wa mahakamani, kesi yao ilitakiwa kusikizwa Jumanne ya tar. 20 Desemba 2011. Kutokana na mvua kubwa ya mafuriko, nikashindwa kufika Kisutu Magistrate hiyo saa mbili ilivyotakiwa, jitihada zangu zote za kusaka habari za kesi yao mtandaoni na kwenye magazeti zikakwama, kuwaona uso kwa macho ikashindikana kwa kuwa hawako tena shuleni, achilia mbali uwezekano wa kufutiwa dhamana waliyowekewa na ex-co-student wenzao wa UDSM, kwani sheria ndogo za chuo haziruhusu mwanafunzi kumdhamini raia kwa mgongo wa Afisi ya Mshauri wa Wanafunzi.
Kwa yeyote mwenye taarifa za mwendelezo wa kesi yao anifahamishe...
Natanguliza shukurani.
 
Heading yako haipo sawa. Unafahamu chuo cha taifa wewe?.
 
Heading yako haipo sawa. Unafahamu chuo cha taifa wewe?.

ndio,
ni Chuo chenye sura ya kitaifa, yaani uwezo wa kuchukuwa idadi kubwa ya wanafunzi kwa kozi nyingi iwezekanavyo, na kiwe kinamilikiwa na serikali kwa asilimia zote bila kusahau kuwa tegemeo la taifa kitaaluma.
Therefore UDSM qualifies to be a State University.
Au wewe una maoni gani?
 
kwenye vyombo vya habari waliandika chuo kikuu. that was specific. udsm. kama ingekuwa tumaini au udom wasingesema chuo kikuu. bali chuo cha.... fill in da blank. sio dharau mkuu ni mazoea tu. teh teh
 
nashukuru kwa ufafanuzi.
Back to the topic...
Any news?
 
unaposema uwezo wa kuchukua idadi kubwa ya wanafunzi umefanya utafiti kweli, kati ya Mlimani na Udom kipi kinachukua idadi kubwa ya wanafunzi! Au udom hakimilikiwi na serikali?

Unaposema serikali inategemea ud kitaaluma unamaanisha nini?. Unataka kuaminisha umma kuwa serikali inategemea wahitimu wa ud pekee. Je SUA na kilimo chake serikali haimtegemei?.

Jarbu kunipa jibu zuri zaidi.
 
nipe vigezo vya kukipa udsm hadhi ya chuo cha taifa.

kwanza ndio kisima cha elimu tanzania,huwez ongelea mafanikio ya elimu bongo bila kuitaja udsm..
 
Heading yako haipo sawa. Unafahamu chuo cha taifa wewe?.
Hajui huyu hata upeo wake wa kufikiri ni mdogo sana. Hajui hatma yao ni kupoteza mwelekeo wa kimaisha kwani hilo ndo lengo kuu la Serikali ya CCM, Kwa mtu yeyote ambaye anamtazamo tofauti na CCM.
 
We unaleta mada kimajigambo haya, kamulize mukandamizwaji or mukandara atakujibu
 
Haka ka mada ka-kipumbavu kameanzishwa na watoto sio wasomi

hapana mkuu.
Michango ya akina mzee ndo imechafua thread... Mimi nina lengo zuri la kujua hatima ya wanafunzi hao 41 walioshtakiwa Kisutu Magistrate Court...
 
hapana mkuu.
Michango ya akina mzee ndo imechafua thread... Mimi nina lengo zuri la kujua hatima ya wanafunzi hao 41 walioshtakiwa Kisutu Magistrate Court...

nakushauri uwe unahudhuria kesi zao pindi zinapotajwa
 
nakushauri uwe unahudhuria kesi zao pindi zinapotajwa

nishasema hapo juu kuwa mvua za mafuriko zilinifanya nishindwe kufika mahakamani Kisutu.
Nimepata taarifa kuwa kesi itaendelea tar. 10 Januari 2012...
By the way, nimetaarifiwa kuwa katika 'hearing' iliyopita hakimu alikataa ombi la Chuo Kikuu kujitoa 'immediately' kwenye udhamini wa washtakiwa...
If other factors remain constant, nitakuwako mahakamani kwenye tarehe tajwa.
 
humu ndani mada imeshawekwa pembeni sasa na kuanza mabishano ya vyuo maana kuna wengine bila ubishi kati ya UDOM na UDSM siku haiwi nzuri
 
humu ndani mada imeshawekwa pembeni sasa na kuanza mabishano ya vyuo maana kuna wengine bila ubishi kati ya UDOM na UDSM siku haiwi nzuri

nadhani nimejitahidi kadiri ya uwezo wangu kuirudisha mada kwenye mstari...
Tunaweza kuendelea kutokea hapo.
Any clues? Mawakili wao, legal position etc etc?
 
ngoja nimuulizie mukandala nitawapa majibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…