Nini hatima ya wenye daraja la nne wanaosomea ualimu vyuo binafsi 2014?

Nini hatima ya wenye daraja la nne wanaosomea ualimu vyuo binafsi 2014?

makwetu

Senior Member
Joined
Jan 19, 2013
Posts
124
Reaction score
28
Serakali imefuta rasmi kidato cha nne wenye ufaulu wa divisheni four ya point 26,27,33 na 34 kusomea ualimu katika vyuo vyake.

Hii ni kutokana na vigezo walivyovitumia katika kuchagua wanafunzi wa kujiunga na vyuo vyake vya ualimu hapa nchini. Wamechukua kuanzia divisheni 1 hadi III tu.

Swali langu, nini hatima ya wale waliobaguliwa na serikali katika awamu hii wanaochukuliwa na vyuo vya watu binafsi? WAZAZI na Wanafunzi wamejawa na hofu kwani hadi sasa serikali halijatoa tamko lolote kuhusiana na hali hiyo.

i watoto wetu wanaosomea shule za kayumba tutawapeleka wapi? watoto wa wakulima watakuwa na uwezo wa kuhimili karo ya mamilioni ya fedha katika vyuo vya watu binafsi?.
 
Either Umeelewa hadi ukapitiliza au hukueelewa kabisa,
kilichopo kuna makundi mawili waliomaliza kidato cha 2013 na waliomaliza nyuma ya hapo.
div 4 ya points 26 na 27 kama umemaliza nyuma ya 2013 bado unasifa na kusomea ualimu,
 
Unachosemema si kweli.Mimi nimewasiliana na chuo kimoja anachoenda mdogo wangu,wizara imetoa maelekezo hakuna wa div.4 aliyechukuliwa pia hakuna certificate tena.
 
mbona mm sielewi hapo jamani kila mtu anayeibuka na lake ebu mtwambie ukweli kuhusu hili.

tatizo hawaweki sorce ya habari zao kama wamefuta mbona walengwa hawapewi taarifa? Kwani hao wakuu wa chuo ndo wanao chagua kwanza kuna vyuo vya certificate kama mpuguso, kinampanda,bustani,
 
mpango kwao ni kwamba hakuna certificate tena bali ni diploma kwa aliyemaliza form four na advance diploma kwa form six thats why wamefanya hivyo na wanakua chini ya Nacte.
 
hata wenye divion 1,2,na 3 wapo huko kwenye vyuo vya private,
lakini cha kujuuliza ni hawaendi sambamba na wale ambao wako kwenye vyuo vya selikari,

private wanaendelea kutoa mafunzo ya certificate , wakati vya selikari wana mfumo mwingine kbs,

itajukuwaje?...............mwenye majibu karibu tafadhari.
 
Samahani na je wale wenye division four ya 32 wanaosoma A-level private hawatapata shida mbeleni?
 
kama huna hizo credits tatu huwezi kujisajiri kufanya mtihani wa f6.
 
Unachosemema si kweli.Mimi nimewasiliana na chuo kimoja anachoenda mdogo wangu,wizara imetoa maelekezo hakuna wa div.4 aliyechukuliwa pia hakuna certificate tena.
Wanasoma mwaka mmoja, kisha wanafanya bridging exam. Wakifaulu wanaendelea mwaka wa pili.
 
tatizo hawaweki sorce ya habari zao kama wamefuta mbona walengwa hawapewi taarifa? Kwani hao wakuu wa chuo ndo wanao chagua kwanza kuna vyuo vya certificate kama mpuguso, kinampanda,bustani,

tambua kwamba hakuna chuo chochote kinachotoa cheti sas hiv. yaan vyuo vyote vilivyokuwa vinatoa cheti sas hiv watatoa ordinaty diploma kwa walimu wa primary na vyote vilivyokua vinatoa diploma ya ordinary vitatoa higher diploma kwa walimu wa secondary. hali halisi ndio hiyo kwa nchi yetu. na kwa vyuo vya private vinavyotoa chet mpaka sas ni kwa ajilia ya walim wa english medium labda otherwise wanawaibia wanafunz wao
 
Kwa ushauri kama una ka division iv ka 32 na ualimu wamezngua,na una credt 3 muda upo unaeza ukaenda private A-level.
 
Back
Top Bottom