Nini hatma ya mkopo benki iliyofilisiwa.

Swelana

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2016
Posts
418
Reaction score
1,259
Habari,
Jamani naomba kusaidiwa kiushauri kuhusu mkopo niliochukua benki fulani ambayo kwa sasa imefilisiwa na serikali.
Mkopo nilikopa mwaka 2012 kwa makubaliano ya kulipa miaka mitatu yaani mpaka 2015,mkopo wa mil 5
Wakati nachukua mkopo nilidhaminiwa na mwajiri wangu ambapo sehemu niliyofanya kazi ilikuwa ni shule ya mmliki wa hiyo benki pamoja na hati ya kiwanja changu ambacho lengo ilikuwa kukopa ili niongezee pesa niliyokuwa nayo na nijenge nyumba na kweli nikafanikiwa nikajenga.

Nilianza kulipa mkopo huo mwaka 2012 mpaka 2013 mwishoni kwa kukatwa kwenye mshahara,bahati mbaya tukashindwana na mwajiri na akawa ameninyima mkataba tena hivyo nikawa kitaa kwa muda kama miezi 8 bila kibarua hivyo sikuwa nimepeleka marejesho wakati huo nimeshalipa kama mil 3.2 na imebaki kama mil 4.8 kwani nilipaswa kulipa mil 8 kwa mkopo wa mil 5.
Sasa baada ya kukaa bila kupeleka marejesho kwa muda wa miezi kama 8 deni likapanda tena mpaka mil 5.4.
Wakati nimeanza kujiajiri nikawa nimefanikiwa kupunguza mpaka likafika mil 4.8 na ghafla ikatangazwa benki hiyo imefilisika so nikaenda kujua hatma ya mkopo nikaelezwa ni lazima niendelee kulipa sawa nikaendelea.
Lakini sasa nina muda kama wa miezi 4 kila nikipeleka marejesho hawanipi risiti za mashine tofauti na fomu ya kujaza kuweka hela na pia wananiambia niendelee kulipa watanipa balance ya kiasi kilichobaki badae kila nikipeleka wananiambia watanipa balance badae.

Sasa waungwana na GT wa Jf limekaaje hili?
Hivi benki iliyofilisiwa kwa waliokopeshwa huwa inakuwaje?
Msaada tutani na sitaki kebehi za kipuuzi.

Swelana.
 
Tambua kuwa malipo yeyote yasiyokuwa na risiti hayatambuliki
 
Banki kama ipo chini ya muflisi, maana yake muflisi anakusanya madeni benki inayodai na kuuza mali na kisha kulipa wadai wa benki. Kwa maana hiyo deni halifi kwa benki kufilisiwa.

Ila kutoa pesa ya rejesho bila risiti wala acknowlegement yoyote KAMA ULIVYOKUWA UNAPEWA TOKA MWANZO, hii inaleta hofu.
 
kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…