Doncho kun
Member
- Jan 11, 2019
- 11
- 10
Sasa ni siku zaidi ya 50 ya kinachoitwa operation ya kijeshi inayofanywa na shirikisho la Urusi ambapo upande unaoshambuliwa (Ukraine) umejaribu kila namna kuzuia mashambulizi makali ikiwa ni pamoja na kuomba mataifa ya Magharibi kuiwekea vikwazo Urusi, kuharibu zana za kivita za Urusi na kulipiga jeshi la Urusi kwa kuingia uwanja wa mapigano.
Hadi sasa zimerekodiwa hasara kubwa kwa pande zote mbili, ambapo nchi hizo zimepoteza wanajeshi, miundombinu ya kijeshi na kirai, vifaa vya kijeshi na raia (kwa upande wa Ukraine) ambao ni nguvu kazi ya taifa.
Swali ni je nini hatima ya taifa la Ukraine kiuchumi na kisiasa baada ya vita hii ambayo kwa kiwango kikubwa imewaacha katika maumivu makubwa?
Je, nini kitarajiwe kutuliza maumivu hayo kutoka nchi za magharibi ambazo zinaonekana zikiunga mkono Ukraine? Je, kujiunga kwa Ukraine kwenye umoja wa ulaya (EU) kutasaidiaje kupooza maumivu hayo?