Nini hii kuhusu analogia na digitali?

Nini hii kuhusu analogia na digitali?

jogoolashamba

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
348
Reaction score
71
Jamani Tz naomba elimu kiduchu! Kuna ugomvi wa jamaa wanaotaka kuwashiwa mitambo ya analogia lakini wawashaji hawataki. Swali: Hivi kuwasha mitambo ya analogia kuna gharama yeyote mpaka kuzue kelele zote hizo? Kwa nini mitambo yote isiwashwe? Mimi nina simu yenye TV na nilikuwa nikiangalia vipindi mbalimbali kwa mobile yangu. Nina hakika viTV vyote vya aina hii havina bao. Kwa nini hatuwashi mitambo yote miwili, analogia na digitali ili na simu zetu ziendelee kuona? Au kuna gharama inayotishia WaTz kulala na njaa?
 
Hata mimi nadhani kuna jambo zaidi kuliko tunalolijua. Wadau wameshasema kuwa wananchi wengi bado hawajawa tayari na mfumo huu wa digital. Hata hivyo hao wanaozima wamekazania tu kuwa hawawashi bila kutoa sababu za msingi? je kuna mahali ambapo wanafaidika kwa wananchi wengi kukosa habari? Je sababu hizi ni za kibiashara au za kisiasa? Hebu tutafakari na tujiulize kuwa ni nani anafaidika hapa na kwa nini?
 
Back
Top Bottom