Nini hofu ya Spika Ndugai kuchukua hatua dhidi ya Wabunge kina mama 19 wanaodaiwa kuwa ni wa CHADEMA?

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Hebu kila GT yeyote aitazame na kuisikiliza video clip hii ya Spika Ndugai Job mwanzo mwisho.

Umeelewa na kujifunza nini baada ya kusikiliza? Kwanini unadhani Spika wa Bunge la JMT ndg Job Ndugai anapata wakati mgumu kuchukua maamuzi sahihi kwa hawa kina mama na badala yake anapiga siasa chafu..?. Hapo nakuachia wewe msomaji..

MTAZAMO WANGU:

1. Ni wazi kuwa mtanange huu ni kati ya Bunge/Spika Ndugai vs CHADEMA na wala si CHADEMA vs Waliokuwa wanachama wake, kina mama 19 wakiongozwa na Halima Mdee.

2. Bunge la JMT ni chombo cha wananchi cha kutunga sheria na kuisimamia serikali. Linajumuisha wabunge wa makundi matano;

å Wa majimbo
å Wa viti maalumu wanawake
å 10 wa kuteuliwa na Rais
å 5 wa kuchaguliwa na BLW - Zanzibar

Kwa mujibu wa sheria zetu na katiba ya nchi, kila mbunge lazima awe amedhaminiwa (tokana) na chama halali cha siasa kilichosajiliwa kisheria.

Kazi ya Spika wa Bunge ni kuhakikisha analitazama na kulisimamia hitaji hili la kisheria na kikatiba kwa nguvu zote.

3. Sasa, kuna watu wanajiita "wabunge wa viti maalumu" wako ndani ya Bunge isivyo halali kwa sababu hawatambuliwi na chama cha siasa chochote.

Chama cha siasa kilichowadhamini, kimejitoa na hakiwatambui tena kuwa ni wanachama wake.

MASWALI YA KUONGOZA MJADALA HUU:

1. Umeitazama na kuisikiliza clip ya video hiyo hapo juu hadi mwisho? Spika Ndugai yuko sahihi? Kwa kiwango gani na kwa vipi?

2. Kwanini unadhani Spika Ndugai amegeuka kuwa wakili mtetezi wa kina mama hawa?

3. Je, ni jukumu la Bunge kumtetea mbunge aliyevuliwa uanachama wake na chama chama chake cha siasa?

4. Kama siyo jukumu la bunge, ni wapi mbunge anapaswa kwenda kutafuta haki yake ya uanachama anapokuwa na mgogoro na chama chake? Jibu ni MAHAKAMANI, au siyo jamani?

5. Kama hivi ndivyo ilivyo, je tunadhani kina Halima Mdee na wenzake hawajui hili? Na Je, Spika Ndugai hajui hili? Nini kipo nyuma ya pazia ya sakata hili?

6. Na mwisho, tujiulize. Spika Ndugai anapatwa na ugumu gani kuchukua maamuzi sahihi juu ya hawa na badala yake anazidi kulifanya jambo hili kuwa gumu na la ovyo zaidi?

7. Je, si kwamba anaogopa kufanya kosa la mwaka 2017 pale alipowafukuza ubunge wanawake 8 wabunge wa viti maalumu wa CUF kwa sababu kama hizihizi zinazowahusu hawa 19 wanaojiita wa CHADEMA?

Wote tunaelewa kuwa, Mara baada ya CUF Lipumba kuwafutia uanachama hawa wanawake 8, alipeleka taarifa kwa Spika wa Bunge la JMT na Spika haraka haraka akawatangazia kukosa sifa ya kuendelea kuwa wabunge.

Haraka haraka akaipa NEC taarifa na NEC haraka haraka kuteua wengine.

Kwa upande wa pili, hawa wabunge 8 walikimbilia mahakamani na mahakama kusitisha uamuzi wa CUF kufuta uanachama wa hawa 8 kwa muda mpaka shauri lao la msingi litakaposikilizwa.

Sote tunajua kilichotokea. Baada ya kurudi kuchukua nafasi yao bungeni, lahaula! wakakuta zimechukuliwa na watu wengine.

Kukawa na sintofahamu kiasi cha kutaka kuzua mgogoro wa kikatiba.

Je, Ndugai anaogopa hiki?

USHAURI KWA SPIKA NDUGAI:

Unaweza kufanya hivi Bwana Spika.

Washauri hao kina mama kukimbilia mahakamani ili kupata "stop order" ya maamuzi ya chama chao kuwafutia uanachama, kisha wataendelea kuwa wabunge wako.

Na wakati wakiisotea/kuipigania hiyo "stop order" mahakamani, usiwe na haraka kuipa NEC taarifa ili iteue wabunge wengine. Kwa kuwa unawahitaji sana wabunge hawa, tumia influence yako kuishawishi Mahakama kuukataa uamuzi wa CHADEMA..

Unachokifanya hiki kwa sasa ni siyo kabisa. Unanajisi katiba ya nchi yetu ukidhani kuwa unailinda...

Aidha huna audacity ya kuingilia maamuzi ya CHADEMA bila kujali walikosea ama la. Mahakama pekee ndiyo yenye mamlaka haya ya kuhoji uhalali wa maamuzi ya CHADEMA...

Washauri watu wako wafuate utaratibu huu. Ukidhani kuwa CHADEMA wataingia kwenye mtego wako huo, utakesha na mwisho wa siku ngoma lazima ikulalie wewe...!
 
Wao kwa wao hawaelewani huko chadema mbowe anajuwa kinachoendelea ili ale ruzuku mnyika hajui chochote ndiyo maana mbowe yuko kimya hebu wajaribu kwenda mahakamani uone watakavyoumbuka hawawezi kwenda mahakamani mbowe ndio aliowaweka.
 
wao kwa wao hawaelewani huko chadema mbowe anajuwa kinachoendelea ili ale ruzuku mnyika hajui chochote ndiyo maana mbowe yuko kimya hebu wajaribu kwenda mahakamani uone watakavyoumbuka hawawezi kwenda mahakamani mbowe ndio aliowaweka
Huna lolote ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani. Ruzuku inatokana na idadi ya kura za urais, na sio hao wabunge kuwa bungeni. Ukilijua hilo uje uendelee na huu utoto wako hapa jukwaani.
 
Shangaa kuna ruzuku inatoka na viti maalum? hatari sn
 
Namuelewa supika, kwa upande fulani. Hapo kuna matumizi mabaya ya pesa za walipakodi. Maana ataulizwa muda wote amewalipa kwa msingi upi?

Kwa hivyo anaombea kitokee kitu ili ionekane kuwa "sasa"(baada ya hiko kitu kutokea) ndio hao covid19 wamepoteza sifa. Moyoni anaomba sana cdm ikae kikao cha kusikiliza rufaa ili apate upenyo wa kujitoa kwenye hilo "tope". Na inaelekea wenye chama kwa sasa hawaungi mkono uwepo wa hao covid19 kwa mbeleko ya supika.
 
Ucjali, CCM wako pamoja na Spika. Wangekuwa wamempigia kura za imani. Sisi wajumbe tunasubiri hongo.
 
Wanasubiria trilioni 2 za mabeberu.

Moja ya sharti lake ni uwepo wa viongozi wa upinzani kwenye kamati za PAC na LAAC.

Wakati Magu anapora chaguzi zote hakujua hilo.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
CCM waliiba kura kijinga kujaza wabunge wa CCM bungeni.

Baada ya kujaza wabunge wa CCM, wakajikuta wanatengwa na mabunge ya Jumuiya ya Madola kwa kutofikia viwango vya diversity. Hata misaada wakakosa.

Sasa hizi jitihada za kuongeza wabunge wa upinzani kwa lazima ni mkakati wa kuonesha bunge lina wapinzani wa kutosha na limefikia viwango vya kimataifa vya mabunge ya Commonwealth na kuweza kukubalika kimataifa.
 
Hebu kila GT yeyote aitazame na kuisikiliza video clip hii ya Spika Ndugai Job mwanzo mwisho.

Umeelewa na kujifunza nini baada ya kusikiliza? Kwanini unadhani Spika wa Bunge la JMT ndg Job Ndugai anapata wakati mgumu kuchukua maamuzi sahihi kwa hawa kina mama na badala yake anapiga siasa chafu..?. Hapo nakuachia wewe msomaji..

MTAZAMO WANGU:

1. Ni wazi kuwa mtanange huu ni kati ya Bunge/Spika Ndugai vs CHADEMA na wala si CHADEMA vs Waliokuwa wanachama wake, kina mama 19 wakiongozwa na Halima Mdee.

2. Bunge la JMT ni chombo cha wananchi cha kutunga sheria na kuisimamia serikali. Linajumuisha wabunge wa makundi matano;

å Wa majimbo
å Wa viti maalumu wanawake
å 10 wa kuteuliwa na Rais
å 5 wa kuchaguliwa na BLW - Zanzibar

Kwa mujibu wa sheria zetu na katiba ya nchi, kila mbunge lazima awe amedhaminiwa (tokana) na chama halali cha siasa kilichosajiliwa kisheria.

Kazi ya Spika wa Bunge ni kuhakikisha analitazama na kulisimamia hitaji hili la kisheria na kikatiba kwa nguvu zote.

3. Sasa, kuna watu wanajiita "wabunge wa viti maalumu" wako ndani ya Bunge isivyo halali kwa sababu hawatambuliwi na chama cha siasa chochote.

Chama cha siasa kilichowadhamini, kimejitoa na hakiwatambui tena kuwa ni wanachama wake.

MASWALI YA KUONGOZA MJADALA HUU:

1. Umeitazama na kuisikiliza clip ya video hiyo hapo juu hadi mwisho? Spika Ndugai yuko sahihi? Kwa kiwango gani na kwa vipi?

2. Kwanini unadhani Spika Ndugai amegeuka kuwa wakili mtetezi wa kina mama hawa?

3. Je, ni jukumu la Bunge kumtetea mbunge aliyevuliwa uanachama wake na chama chama chake cha siasa?

4. Kama siyo jukumu la bunge, ni wapi mbunge anapaswa kwenda kutafuta haki yake ya uanachama anapokuwa na mgogoro na chama chake? Jibu ni MAHAKAMANI, au siyo jamani?

5. Kama hivi ndivyo ilivyo, je tunadhani kina Halima Mdee na wenzake hawajui hili? Na Je, Spika Ndugai hajui hili? Nini kipo nyuma ya pazia ya sakata hili?

6. Na mwisho, tujiulize. Spika Ndugai anapatwa na ugumu gani kuchukua maamuzi sahihi juu ya hawa na badala yake anazidi kulifanya jambo hili kuwa gumu na la ovyo zaidi?

7. Je, si kwamba anaogopa kufanya kosa la mwaka 2017 pale alipowafukuza ubunge wanawake 8 wabunge wa viti maalumu wa CUF kwa sababu kama hizihizi zinazowahusu hawa 19 wanaojiita wa CHADEMA?

Wote tunaelewa kuwa, Mara baada ya CUF Lipumba kuwafutia uanachama hawa wanawake 8, alipeleka taarifa kwa Spika wa Bunge la JMT na Spika haraka haraka akawatangazia kukosa sifa ya kuendelea kuwa wabunge.

Haraka haraka akaipa NEC taarifa na NEC haraka haraka kuteua wengine.

Kwa upande wa pili, hawa wabunge 8 walikimbilia mahakamani na mahakama kusitisha uamuzi wa CUF kufuta uanachama wa hawa 8 kwa muda mpaka shauri lao la msingi litakaposikilizwa.

Sote tunajua kilichotokea. Baada ya kurudi kuchukua nafasi yao bungeni, lahaula! wakakuta zimechukuliwa na watu wengine.

Kukawa na sintofahamu kiasi cha kutaka kuzua mgogoro wa kikatiba.

Je, Ndugai anaogopa hiki?

USHAURI KWA SPIKA NDUGAI:

Unaweza kufanya hivi Bwana Spika.

Washauri hao kina mama kukimbilia mahakamani ili kupata "stop order" ya maamuzi ya chama chao kuwafutia uanachama, kisha wataendelea kuwa wabunge wako.

Na wakati wakiisitea/kuipigania hiyo "stop order" mahakamani, usiwe na haraka kuipa NEC taarifa ili iteue wabunge wengine..

Unachokifanya hicho siyo. Unajisi katiba. Aidha huna audacity ya kuingilia maamuzi ya CHADEMA bila kujali walikosea ana la. Mahakama pekee ndiyo yenye mamlaka hiyo.
Ndugai analazimisha kuwa na Kambi rasmi ya upinzani bungeni huku waliiba kura bila kutumia akili zake
 
Wao kwa wao hawaelewani huko chadema mbowe anajuwa kinachoendelea ili ale ruzuku mnyika hajui chochote ndiyo maana mbowe yuko kimya hebu wajaribu kwenda mahakamani uone watakavyoumbuka hawawezi kwenda mahakamani mbowe ndio aliowaweka.
Pumbavu hauna akili wala ufahamu..
Ruzuku katika Chama cha Siasa inatolewa kutokana na percentage ya kura za URAIS Chama husika kilichozipata katika Uchaguzi..
Kajipange upya ngumbaru.
 
Huna lolote ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani. Ruzuku inatokana na idadi ya kura za urais, na sio hao wabunge kuwa bungeni. Ukilijua hilo uje uendelee na huu utoto wako hapa jukwaani.
Kura zipi za urais unazozungumzia? Kwani kuna Uchaguzi Mkuu wowote "HALALI" uliofanyika Tanzania hivi karibuni? Ahahahahahahahah!!!!!!!!
 
Hizo kura zilizotangazwa ni baada ya yule shetani aliyeko motoni kuamua zitangazwe hizo, ila zilikuwa nyingi kwelikweli mpaka shetani akachanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom