yuleMskinny
JF-Expert Member
- Sep 22, 2017
- 242
- 136
Kama si mara moja basi mbili au hata zaidi wengi wetu tumewahi kusingiziwa kwa vitu ambavyo hatujawahi kufanya. Either na wazazi wetu, walimu, viongozi na hata marafiki zetu.
Adhabu ya viboko ilifuata au kuvunjika kwa urafiki na inauma sana moyo kuona una chapwa kwa kitu ambacho hujafanya. Sasa kama uliumia kwa hilo, Jiulize wali waliofungwa magereza kwa kesi za kusingiziwa au kesi ambayo ushahidi unaonyesha yeye ni mshiriki ila hakushiriki?
Mara nyingi mahakama zimekua zikihukumu watu wasio na hatia na kuwaweka nyuma ya nondo kwa muda mrefu sana ndo wanakuja kutambua hawakua na hatia.
Je, vipi kama hukumu iliyotolewa ilikua ni ya kifo? Je aliepoteza maisha kwa upungufu ama ushahidi wa kupandikiza inakuaje?
Endelea kusoma na utapata picha ninachotaka kukuambia...
Henry Gleeson
Jamaa huyu alikua shambani kwa mjomba ake akifanya shughuli zake za kila siku alipokuta mwili wa mwanamke aliekua jirani yao ambae alikua mama wa watoto 7. jamaa huyu alitoa taarifa polisi na kibao kilimgeukia yeye kua ndo muuaji na huenda alifanya hivo kuficha mahusiano yake yeye na mwanamama huyo. Jamaa huyu alihukumiwa kifungo cha maisha na baada ya kufa alizikwa huko huko magereza aliekuepo. Miaka mingi badae marafiki na watu wakaribu walikamilisha upelelezi wao kwa kugundua kwamba jamaa hakua na hatia.
Carlos DeLuna
February 1983, watu walishuhudia mwanaume mmoja akichomwa visu mpaka kufa karibu na kituo cha mafuta huko Texas, watu wale walitoa maelezo ili kuwasaidia polisi na maelezo yao yalikua yalifit profile ya bwana Carlos DeLuna. Baada ya Carlos kukamwata hakukubali kosa na alisema huenda ikawa ni Carlos Hernandez mwanaume mwingine ambae walifanana sana hata wakati mwingine watu walizani ni mapacha. Mahakama ilikataa uwepo wa Carlos Hernandez na ilimuhukumu Carlos Deluna Kifo cha sindano ya sumu. Miaka kadhaa badae iligundulika kua ni kweli Carlos Hernandes yupo na alikua amefungwa na kufia magereza moja huko marekani. Wafungwa wenzake walisema kua walikua wakimsikia kila siku akisema kua aliua mtu na kesi akabeba fala mwingine.
Hizo na zingine nyingi ni baadhi ya hukumu hatari ambazo kwa kutumia jina la mahakama watu wasio na hatia waliuwawa.
Kubwa zaidi ni kijana GEORGE STINNEY JR. Kijana huyu alinyongwa akiwa na umri wa miaka 14 tuu kwa kesi ya kuuwa watoto wakike wawili miaka 11 na 7 baada ya kutaka kuwabaka na kushindwa (Kama mahakama ilivoamua kujiridhisha) George (Mtu mweusi) alihukumiwa huko north Carolina mwaka 1944 ambapo ubaguzi wa rangi haukuruhusu watu weusi kuingia mahakamani labda tu awe muhalifu. Kesi ya George iliendeshwa na jopo la mawakili weupe tuu na ndani ya dakika 10 tuu hukumu ya kifo kwa shoti ya kiti cha umeme ilitolewa kwa George.
Miaka 70 baadae walikuja kujua kwamba George hakua na hatia.
Je hii inamsaidia nini George? Je familia ya George inapata pole gani kwa upuuzi huu uliofanywaa na mahakama? Dada yake sasa ni mtu mzima kabisa wa makamo na hii kitu amesema hatawahi kusamehe moyoni mwake.
MBALI NA HUKUMU ZA KIFO WAKO WATU WANAKULA NYUNDO KADHAA JELA KWA KESI ZA KUPAKAZIWA AU KUSUKWA. HII INASIKITISHA SANA. JE? UNAIONAJE HII WEWE KWA UPANDE WAKO?