Haya nafikiri yameshawahi kujadiliwa humu! Nafikiri wana JF wengi humu wanasisitiza kuwepo na ustawi wa mambo yanayo wagusa watanzania, na mimi nakubali, kwa sababu haya ya ufisadi sasa si news! Changamoto ni nyingi.
Pia nafikiri kuwepo angalau ka wiki kamoja kila mwezi ambao wana JF watachangia kwa umahiri mambo endelevu yote kutoka Utamaduni mpaka Siasa.
Kuwepo na category zote kama maazimio ya biashara na hata vyama vya siasa(maazimio yenye malengo ya kukuza Utamaduni na Siasa na n.k),jinsi ya kukwepa yale yaliyotokea muhimbili,municipal planning,reverse engineering(what is possible?), water shoratge(tuna bahari, na ma-ziwa), tunawezaje kutumia tekelinalokujia la sasa kubadilisha maji chumvi, utumiaji wa mionzi ya jua kwa ajili ya umeme sehemu zilizo mbali na miji au vijiji na kadha wa kadha...kama wana JF wanavyosema!
Changamoto Tanzania ni kabambe!! Siasa tuwaachie waliopo ulingoni na sisi tuwaachie changamoto kabambe kwa kuwa Mavisionary!! wana Vision mpo?