JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Wanawake wamekuwa wakikumbana na kebehi, matusi na hata vipigo kutoka kwa wakunga wakati wa kujifungua.
Utafiti uliofanywa na WHO ulibaini kwamba wanawake wenye umri mdogo, na walio na kiwango cha chini cha elimu wako hatarini kuteswa kupitia kunyanyapaliwa, kubaguliwa, kufanyiwa taratibu za kitabibu bila ya hiari yao au kutelekezwa.
WHO inasema msaada kutoka kwa mkunga wakati mjamzito anajifungua una mchango kati ya uhai na kifo huduma bora za mkunga huokoa maisha ya mzazi.
Unafikiri ni kwanini Wakunga hukebehi, kutukana au hata kupiga wajawazito?
Upvote
0