Nini hupelekea Rushwa kwenye Sekta ya Afya

Nini hupelekea Rushwa kwenye Sekta ya Afya

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
rushwa.png

Chuo cha Basel kilifanya utafiti kwenye nchi tatu za Afrika Mashariki (Tanzania, Uganda na Rwanda) kuhusu Rushwa kwenye utoaji wa huduma ya afya.

Ilibainika tatizo hilo limetokana na kusuasua kwa sekta ya afya katika nchi hizo na kusababisha upatikanaji wa huduma kuwa mgumu.

Aidha kupatiwa huduma kulingana na namna unavyofahamiana na mtoa huduma kumepelekea watu kutafuta huduma sehemu wanazofahamiana na watoa huduma na kama hakuna anayemfahamu hutoa pesa kujenga ukaribu na mtoa huduma.

Pia Rushwa imeendelea kuota mizizi kutokana na watu kuchukulia kuwa ni jambo ambalo lipo haliepukiki na ni la kawaida.

Kuimarisha huduma za afya katika nchi hizo kutapelekea upatikanaji wa huduma kwa urahisi na kupunguza Rushwa na upendeleo.

Lakini pia elimu kuhusu madhara ya Rushwa ni muhimu ili kuhakikisha watu wanaacha kuona kuwa Rushwa haiepukiki.
 
Upvote 0
Urahisi wa kupata huduma yoyote ile kutaondoa rusha automatically.

Kusema tu Watu wapewe elimu madhara ya rushwa sidhani kama inatosha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom